Magonjwa ya ndani ya mwili

UGONJWA WA POLIO/UGONJWA WA KUPOOZA

Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko

Maelezo ya jumla

Ugonjwa wa polio ni ugonjwa unaoathiri mishipa ya fahamu na kusababisha kupooza. Ugonjwa huu husababishwa na virusi (poliovirus) wanaoishi kwenye mfumo wa kumeng’enya chakula. Si kila mtu anayeambukizwa virusi hivi vya polio hupooza, watu wengi huwa na dalili za kawaida tu, kama; maumivu ya kichwa, homa, kutapika, maumivu ya mgongo, maumivu ya misuli, kukaza kwa misuli na kuwashwa ngozi na kisha hupona. Watu ambao hawajapata chanjo dhidi ya polio na wanaosafiri kwenda katika maeneo yenye mlipuko, wako katika hatari zaidi ya kuambukizwa.

Utambuzi hufanyika baada ya vipimo kufanyika. Kama ilivyo kwa magonjwa mengine yanayosababishwa na virusi, hakuna dawa ya kuponya ugonjwa wa polio. Madaktari hujaribu kudhibiti dalili mpaka maambukizi yatakapopona yenyewe. Matarajio ya kupona hutegemea ugonjwa umejitokezaje. Kama uti wa mgongo na ubongo havitaathiriwa, 90%  hupona kabisa.

Nini dalili za ugonjwa wa polio?

Ugonjwa wa polio hujitokeza kwa namna tatu baada ya mtu kuambukizwa:

 • Maambukizi yasio makali
 • Maambukizi makali yasiyosababisha kupooza
 • Maambukizi makali yanayosababisha kupooza

Maambukizi yasio makali

ugonjwa unapojitokeza kwa namna hii, mgonjwa anaweza asiwe na dalili yoyote au anaweza kupata dalili za kawaida tu, takribani 95% ya watu wanaoambukizwa ugonjwa huu hupata namna hii ya polio. Mgonjwa anaweza kuwa na dalili zifuatavyo;

Watu wenye maambukizi ya polio yasio makali, wanaweza wasipate dalili yoyote, na hata  kama wakipata dalili, dalili huzidumu kwa zaidi ya saa 72.

Maambukizo makali yasiyosababisha kupooza

Maambukizi makali ya polio huathiri ubongo na uti wa mgongo.
Maaambukizo makali ya polio yasiyosababisha kupooza huwa na dalili zifuatazo

Dalili hizi kwa kawaida hudumu kwa wiki 1 – 2.

Maambukizi makali yanayosababisha kupooza

Huwa na dalili zifuatazo;

 • Homa huanza siku 5 – 7 kabla ya dalili nyingine
 • Kupungua kwa uwezo wa kuhisi wa eneo fulani (lakini si kupoteza hisia kabisa)
 • kuvimbiwa
 • Kupata shida kupumua
 • Kupata shida kumeza
 • Kufunga choo
 • Kupata shida / ugumu kukojoa
 • Kutokwa na mate mengi
 • Maumivu ya kichwa
 • Kukasirika kasirika sana
 • Kukaza au kukakamaa kwa misuli ya miguu, shingo au mgongo
 • Maumivu ya misuli
 • Kulegea kwa misuli- hii hutokea upande mmoja tu, au upande mmoja unaweza kuwa umeathirika zaidi kuliko mwingine
 • Hii hutoka haraka sana
 • Mahala panapolegea/kuishiwa nguvu hutegemea sehemu ya uti wa mgongo iliyoathiriwa
 • Baadae sehemu iliyolega hupooza kabisa
 • Mgonjwa hupata maumivu hata ukimgusa kidogo tu

Ugonjwa wa polio husababishwa na nini?

Ugonjwa wa polio unaosababishwa na maambukizi ya virusi vya polio. Virusi hivi hupatikana kwenye mate, kamasi au kinyesi cha mtu aliyeambukizwa. Polio huambukizwa toka kwa mtu mmoja mpaka mwingine. Virusi huingia mwilini kupitia kinywani au puani. Huanza kuzaliana kooni na kwenye mfumo wa kumeng’enya chakula. Kisha hufyonzwa na kuingia kwenye mfumo wa damu na kusafirishwa mwili mzima. Dalili za ugonjwa huanza kuonekana kuanzia siku ya 5-35 baada ya maambukizi.

Nani yuko kwenye hatari zaidi za kupata ugonjwa wa polio?ugonjwa wa polio

Watu walio kwenye hatari zaidi ya kuambukizwa polio ni wale:

 • Ambao hawajapata chanjo dhidi ya polio na wako katika eneo lenye kiwango kikubwa cha maambukizo
 • Ambao wanasafiri kwenda kwenye maeneo yenye mlipuko wa polio

Katika maeneo yenye mlipuko, makundi yaliyo katika hatari zaidi ya kuambukizwa ni pamoja na watoto, wanawake wajawazito na wazee. Kati ya mwaka 1840 na mwaka 1950, polio ilikuwa janga la dunia, watu wengi sana waliathirika. Lakini tangu chanjo ya polio kupatikana, ugonjwa huu umepungua kwa kiasi kikubwa. Katika baadhi ya nchi duniani ugonjwa huu umetokomezwa kabisa. Watoto katika nchi nyingi ikiwemo Tanzania hupewa chanjo wakiwa wadogo. Kwa sababu ya juhudi za shirika la afya duniani na serikali za mataifa yote, ugonjwa huu umepungua sana. Kuna matukio machache tu yanayotokea katika nchi za Afrika na Asia.

Wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Mwone mtoa huduma ya afya kama:

 • Mtu wa karibu yako amepata polio na haujapata chanjo dhidi ya polio
 • Unaanza kupata dalili za polio
 • Kama mwanao hajapata chanjo ya polio

Utambuzi wa ugonjwa wa polio

Vipimo vinavyoweza kufanyika ni pamoja na:

 • Uchunguzi wa sampuli inayochukuliwa kwa sindano kwenye uti wa mgongo- Cerebral spinal fluid
 • Kupima kiwango cha kingamwili (antibodies) kinachotengenezwa kama umeambukizwa virusi vya polio
 • Kuchukua sampuli kooni, kwenye uti wa mgongo au kinyesi na kukipima

Uchaguzi wa matibabu

Hakuna dawa ya kuponya polio. Lengo la matibabu ni kudhibiti dalili mpaka maambukizi yatakapoisha yenyewe. Watu wenye maambukizi makali wanaweza kuhitaji msaada ili kuokoa maisha yao, hasa wakipata shida kupumua. Matibabu ya polio hutegemea makali ya dalili za mgonjwa. Matibabu yanaweza kujumuisha:

 • Antibiotiki kwa ajili ya kutibu maambukizi kwenye njia ya mkojo
 • Madawa (kama vile bethanechol) ya kusaidia mkojo kutoka kwenye kibofu – kwa wagonjwa wenye matatizo ya kukojoa
 • Kukandwa kwa taulo au kitambaa cha joto ili kupunguza maumivu ya misuli
 • Dawa za maumivu ili kupunguza maumivu ya kichwa, maumivu ya misuli, na kukakamaa kwa misuli.
 • Mazoezi ya mwili, viatu maalumu au upasuaji wa mifupa ili kusaidia kurejesha nguvu kwenye misuli

Nini cha kutarajia?

Matarajio ya kupona hutegemea;

 • ugonjwa umejitokezaje (Maambukizi yasiyo makali, maambukizi makali yasiyosababisha kupooza au maambukizi makali yanayosababisha kupooza)
 • Sehemu ya mwili iliyoathirika

Kama ubongo na uti wa mgongo havitaathiriwa, na karibia 90% ya wagonjwa hawaathiriwi, hupona kabisa. Ni dharura kama ubongo na uti wa mgongo vitaathiriwa. Mgonjwa anaweza kupooza na hata kufa (Hasa kutokana na matatizo ya kupumua). Ni kawaida kwa wagonjwa kulemaa na si kufa. Maambukizi kwenye sehemu ya juu ya uti wa mgongo au ubongo huongeza hatari ya kupata matatizo ya kupumua.

Matatizo yanayoweza kutokea

Kuzuia ugonjwa wa polio

Chanjo ya polio hufanya kazi kwa ufanisi mkubwa. Inaweza kukinga zaidi ya 90% ya maambukizi

MAELEZO KWA MUHTASARI KUHUSU POLIO

Maelezo ya jumla

Ni maambukizi virusi ambayo kwa kawaida yanatambuliwa kwa kusababisha kupooza

Sababu za ugonjwa wa polio

Virusi vya polio (aina ya I, II na III)

Epidemiolojia ya ugonjwa wa polio

Ugonjwa huu ulitokea duniani kote kabla ya enzi za chanjo. Visa vya ugonjwa wa polio vinaweza kutokea kwa makundi au kama mlipuko. Ni ugonjwa unaowaathiri zaidi watoto. 70 -80% ya wagonjwa wana umri chini ya mika 3. Karibu 90% ya watu wote wanaoam bukizwa hawapati dalili yoyote. Kupooza kunatokea kwa chini ya 1% ya watu wote walioambukizwa.

Uambukizo wa ugonjwa wa polio

Kwa kawaida ni kati ya mtu na mtu, kwa kushika mikono au kula chakula kilichochafuliwa au kuandaliwa na mtu ambaye hajaosha mikono vizuri baada ya kushika kinyesi.

Muda kabla ya dalili kuanza kuonekana

Kwa kawaida siku 7-14

Muda wa uambukizo wa ugonjwa wa polio

Muda haufahamiki kwa uhakika, ila kumwambukiza mtu mwingine kunawezekana kama bado virusi wanatolewa kwenye kinyesi

Nani yuko kwenye hatari

Watoto wako kwenye hatari zaidi lakini kupooza kunatokea kwa nadra. Ukisha pata maambukiz mara moja, unapata kinga ya kudumu maisha yote.

Dalili za ugonjwa wa polio

 • Kwa kawaida hakuna dalili kabisa au unapata homa pekee kwa 90% ya watu walioambukizwa
 • Kama ugonjwa ukiendelea na kuwa mkali, utapata maumivu makali ya misuli, kukaza kwa shingo na mgongo na kupooza kunaweza kutokea
 • Kupooza hakuna dalili yoyote na kunatokea ndani ya siku 3-4 za ugonjwa
 • Miguu inaathirika zaidi kuliko sehemu nyingine za mwili
 • Kupooza kwa misuli ya kupumua na kumeza chakula kunaweza kutishia maisha

Utambuzi wa ugonjwa wa polio

Kwa kuangalia dalili na data za kiepidemiolojia

Matibabu

Kwa kuangalia dalili alizonazo mgonjwa na kuzitibu

Kuzuia

 1. Elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kuwapatia chanjo watoto
 2. Kupokea chanjo ya polio baada ya kuzaliwa
 3. Kuzingatia matumizi sahihi ya choo

Vyanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/001402.htm

  • 2 years ago (Edit)

  Asante nitawafundisha wengi kuhusu huu ugonjwa

   • 2 years ago

   karibu na asante

Leave feedback about this

 • Quality
 • Price
 • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X