UGONJWA WA LUPUS :Sababu, dalili, matibabu

Ugonjwa wa lupus ni nini?

Ugonjwa wa lupus ni ugonjwa wa kinga ya mwili unaoweza kuathiri sehemu nyingi za mwili. Kwa kawaida, mfumo wa kinga ya mwili hutengeneza antibodies ambazo hutumika kutukinga na maambukizi. Kwa watu wenye ugonjwa wa lupus, mfumo wa kinga ya mwili unakanganyika na kutengeneza antibodies ambazo hushambulia na kuharibu seli na tishu za mwili wako wenyewe kimakosa.ugonjwa wa lupus

Nani anapata lupus?

Ugonjwa wa lupus unaweza kumpata mtu yeyote, lakini unawapata zaidi wanawake walio na umri kati ya miaka 15 na 44. Wanawake Weusi, wenye asili ya kihispania, watu wa asia na wamarekani Weusi wana uwezekano mkubwa wa kuwa na ugonjwa huu.ugonjwa wa lupus

Ni zipi dalili za ugonjwa wa lupus?

Sio kila mtu mwenye ugonjwa wa lupus ana dalili sawa na mwingine. Dalili zinaweza kuja na kuondoka, na mara nyingi zinapotea kabisa kwa muda. Dalili zinapoanza au zinapoongezeka ukali, hali hii tunaitaa -shambulio. Dalili za kawaida ni pamoja na:

Lupus inatibiwaje?

Hakuna dawa au chanjo ya kuponya kabisa ugonjwa huu, lakini matumizi ya dawa na mabadiliko ya mfumo wa maisha yanaweza kusaidia kudhibiti dalili ili uishi maisha kamilifu. Aina ya matibabu inategemea sana dalili ulizonazo. Kama una maumivu ya viungo, maumivu ya misuli, au una upele, daktari anaweza kushauri utumie dawa za maumivu kama vile ibuprofen. Dawa zinazotumiwa kutibu ugonjwa wa malaria zinaweza pia kusaidia kupunguza dalili za ugonjwa wa lupus na kupunguza uwezekano wa kupata shambulio. Dawa aina ya steroid zinaweza pia kusaida kupunguza uvimbe. Kwa sababu ya hatari ya madhara mabaya ya dawa unazotumia, wakati mwingine daktari atakutaka uache kutumia aina fulani ya dawa kama dalili zimepungua. Ni muhimu kuonana na daktari mara kwa mara kwa uchunguzi.

Kumbuka; Aina ya matibabu utakayopata yatalenga kuzuia mashambulio ya ugonjwa yasitokee, na kama yakitokea kuyadhibiti na mwisho kabis, kuzuia viungo vya mwili visiharibiwe na ugonjwa.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/lupus.html

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi