UGONJWA WA MIONZI: Sababu, dalili, matibabu

Maelezo ya jumla

Ugonjwa wa mionzi (radiation injury) husababisha dalili kwa sababu ya kukutana na mionzi kwa kiasi kikubwa.

Kuna aina kuu mbili za mionzi: mionzi isiyoumiza (nonionizing) na mionzi inayoumiza (ionizing).

 • Mionzi isiyoumiza (nonionizing) ni mionzi inayotokana na mwanga, mawimbi ya radio, mawimbi ya vifaa vya umeme na radar. Aina hii ya mionzi kwa kawaida haisababishi uharibifu kwa tishu za mwili.
 • Mionzi inayoumiza (ionizing) ni aina ya mionzi inayosababisha uharibifu papo hapo inapokutana na tishu za mwili, miali ya eksirei, miali ya gamma, na miali mingine ya sehemu za atomu (mwali wa nyutroni, mwali wa elektroni, mwali wa protoni, meson, na mingine) inayotoa mionzi inayoumiza. Aina hii ya mionzi inaweza kutumika katika vipimo vya kitabibu na matibabu, viwanda na kwenye shughuli za uzalishaji, silaha za kivita na utengenezaji wa silaha za kivita, na mambo mengine.

Mambo ya kuzingatiaugonjwa wa mionzi

Ugonjwa wa mionzi unatokea mwanadamu (au mnyama) anapokutana na kiwango kikubwa cha mionzi inayoumiza.

Kukutana na mionzi kunaweza kuleta matatizo kama utakutana na mionzi kiasi kikubwa kwa wakati mmoja, au kwa kukutana na mionzi kiasi kidogo kidogo kwa muda mrefu. Kukutana na mionzi kunaweza kutokana na ajali au kwa makusudi (kama kitendo cha tiba ya mionzi)

Ugonjwa wa mionzi kwa kawaida unatokea zaidi kwa kukutana na miozni mingi kwa wakati mmoja na kusababisha dalili zinazofuatana. Unapopigwa na kiasi kidogo kidogo cha mionzi kwa muda mrefu, dalili huwa zinachelewa sana na uwezekano ni mkubwa wa kupata matatizo baadae kama kansa, kuwahi kuzeeka, na hii inaweza kutokea kwa muda mrefu.

Hatari ya kupata ugonjwa wa kansa unategemea kiwango cha mionzi unachokutana nacho, na kinaweza kujikusanya mwilini kwa muda mrefu. Hakuna kiwango kidogo kwenye mionzi.

Kukutana na miali ya eksirei (x-ray) au mionzi ya gamma (gamma rays) hupimwa kwa roentgens. Kwa mfano:

 • Kama mwili mzima utapokea kiwango cha 100 roentgens/rad (au 1 Gy) kitasababisha ugonjwa wa mionzi
 • Kama mwili mzima utapokea kiwango cha 400 roentgens/rad (au 4 Gy) kitasababisha ugonjwa wa mionzi na kifo kwa nusu ya watu. Bila matibabu, karibia kila mtu anayepokea kiwango cha mionzi zaidi ya hiki atakufa ndani ya siku 30.
 • Kupokea kiwago cha 100,000 roentgens/rad (1000 Gy) husababisha mtu kupoteza fahamu papo hapo na kifa ndani ya saa 1.

Ukali wa dalili na ugonjwa unategemea aina na kiasi cha mionzi, kwa muda gani umekutana na mionzi, na ni sehemu gani ya mwili iliyopigwa mionzi. Dalili za ugonjwa wa miozi zinaweza kutokea papo hapo baada ya kukutana na mionzi, au ndani ya siku, wiki au miezi. Uroto wa mifupa na mfumo wa kumeng’enya chakula unaharibiwa kirahisi sana na mionzi. Watoto wachanga na watoto waliotumboni mwa mama wako kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa mionzi wenye dalili kali.

Kwa sababu ni ngumu kutambua ni kiasi gani ya mionzi kimeupiga mwili wakati wa ajali za nyukilia, njia bora zaidi ya kupima ukubwa wa kiwango cha mionzi mwili uliopokea ni kwa kuangalia muda uliotumia toka ulipopata ajali mpaka dalili zilipoanza, ukali wa dalili, na mabadiliko ya seli nyeupe za damu. Kama mtu akitapika damu  ndani ya saa moja baada ya kupata mionzi, hii huwa inamaanisha kiwango cha mionzi alichopokea ni kikubwa sana na kifo kinategemewa.

Watoto wanaopokea tiba mionzi au wanaokutana na mionzi kwa ajali watatibiwa kwa kufuatilia dalili na hesabu ya seli za damu. Kufanya uchunguzi wa seli za damu mara kwa mara ni muhimu na kipimo hiki kinahiji kutoa damu kwenye mshipa mara kwa mara.

Ni zipi dalili za ugonjwa wa mionzi?

Zifuatazo ni baadhi ya dalili na ishara zinazoweza kujitokeza kama umekutana na mionzi

Daktari atakushauri namna bora ya kutibu dalili hizi. Dawa zinaweza kutolewa ili kupunguza kichefuchefu, kutapika na maumivu. Unaweza kuongezewa damu kama una upungufu wa damu. Dawa za antibiotiki hutumika kuzuia na kupambana na maambukizi.

Ni nini sababu ya ugonjwa wa mionzi

Sababu za ugonjwa mionzi ni pamoja na:

 • Kukutana n kiwango cha juu cha mionzi kwa sababu ya ajali kama vile kwenye kinu cha kufua umeme wa nyukilia
 • Kukutana au kupigwa mionzi kiwango kikubwa zaidi ya inavyohitajika wakati wa tiba mionzi

Uchaguzi wa matibabu ya ugonjwa wa mionzi

Huduma ya kwanza

 • Kagua kama mgonjwa anapumua na kama mapigo ya moyo yapo
 • Anza kufanya CPR, kama inahitajika
 • Mvue nguo mtu aliyekutana na mionzi na uziweke katika chombo maalumu chenye mfuniko. Hii itasaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira kwa mionzi.
 • Osha vizuri mwili wa mgonjwa kwa kutumia sabuni
 • Kausha mwili na kuufunika kwa blanketi laini na safi
 • Piga simu au mpeleke mgonjwa kwenye kituo cha afya kilicho karibu kama unaweza kufanya hivyo bila kuongeza hatari kwako na kwake

TOA TAARIFA KUWA NI UGONJWA WA MIONZI KWA WATAALAMU WA AFYA AU WAHUDUMU WA DHARURA MARA TU UNAPOFIKA AU WANAPOFIKA ULIPO

 • Kama dalili zikitokea wakati au baada ya matibabu ya kutumia mionzi:
 • Ongea na mtaalamu wa afya au nenda haraka kwenye kituo cha afya kilicho karibu yako
 • Kuwa makini na mahala palipoathirika
 • Tibu au hudumia ugonjwa wa mionzi kama ilivyopendekezwa na daktari

USIFANYE YAFUATAYO

 • USIBAKIE mahala penye mionzi
 • USIPAKE mafuta au dawa kwenye maeneo yaliyopigwa na mionzi
 • USIBAKIE ukiwa umevaa nguo ulizokuwa nazo wakati unakutana na mionzi

Kuzuia ugonjwa wa mionzi

 • Epuka kukutana na mionzi bila sababu ya msingi
 • Watu wanofanya kazi katika maeneo hatari yenye mionzi, wanapaswa kuvaa vitambulisho au vifaa maalumu vinavyopima kiwango cha mionzi iliyoko kwenye mazingira na inayofikia miili yao
 • Sehemu za mwili ambazo hazihusiki kwenye matibabu ya mionzi zinapaswa kufunikwa vizuri ili zisipatwe na mionzi wakati wa matibabu au wakati wa kupigwa picha ya eksirei au tiba mionzi.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/000026.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi