UGONJWA WA MOYAMOYA: Sababu, dalili, matibabu

Maelezo ya jumla

Ugonjwa wa moyamoya ni ugonjwa nadra sana, unasababishwa na matatizo yanayoendelea ya mfumo wa kuzungusha damu yanayotokana na kuziba kwa mishipa ya ateri inayopeleka damu kwenye ubongo sehemu inayoitwa basal ganglia.

Jina “moyamoya” linamaanisha “puff ya moshi unaotolewa baada ya kuvuta tumbaku” kwa lugha ya kijapani na inaelezea mwonekano wa mwingiliano wa vishipa vidogovidogo vinavyotengenezeka kama mbadala wa njia ya damu kupita baada ya mishipa mikubwa kuziba.

Ugonjwa wa moyamoya ulitambuliwa kwa mara ya kwanza nchini japana miaka ya 1960 na mpaka sasa umepatikana kwa wagonjwa nchini Marekani, Ulaya, Australia, na Afrika. Ugonjwa huu unawaathiri zaidi watoto, lakini unaweza pia kuwaathiri watu wazima.

Ni zipi dalili za ugonjwa wa moyamoya?Ugonjwa wa moyamoya

Zifuatazo ni baadhi ya dalili za ugonjwa wa moyamoya:

Ni nani yuko kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa wa moyamoya?

Ugonjwa huu unatokea zaidi kwenye familia zenye historia za ugonjwa huu, watafiti wanadhani kuwa, ugonjwa wa moyamoya ni matokeo ya kurithi jeni zenye matatizo.

Ni wakati gani unapswa kutafuta usaidizi wa kitabibu?

Mpeleke haraka mgonjwa kwa daktari kama ana dalili yoyote kama iliyotajwa hapo

Utambuzi wa ugonjwa wa moyamoyaugonjwa wa moyamoya

Daktari atafanya uchunguzi na kupendekeza baadhi ya vipimo ili kusaidia utambuzi wa tatizo hili

  • Vipimo vya damu- ili kuangalai uwezo wa damu kuganda
  • Vipimo vya uwezo wa kufanya kazi wa tezi dundumio (tezi ilio sehemu ya mbele ya shingo)
  • Picha ya Ct scan: Picha hizi husaidia kutambua kama kuna damu inavuja kwenye ubongo
  • Kipimo cha cerebral angiography: hiki husaidia kutambua kama kuna uzibe kwenye mishipa inayopeleka damu kwenye ubongo

Uchaguzi wa matibabu

Kuna aina nyingi za upasuaji zinazosaidia kurejesha mzunguko wa damu kwenye sehemu ya ubongo iliokosa damu baada ya kuziba kwa mishipa ya ateri. Watoto kwa kawaida huitikia vyema tiba ya upasuaji zaidi ya watu wazima, lakini wagonjwa wengi hawapati tena kiharusi au matatizo mengine baada ya upasuaji.

Matarajio

Kama upasuaji usipofanyika, wengi wa watu wenye ugonjwa wa moyamoya hupata matatizo ya kupungua kwa uwezo wa kufikiri na akili kwa sababu ya kupata mashambulio kadhaa ya ubongo/ kiharusi kadri ugonjwa unavyoendelea kuwa mbaya zaidi kwa kuziba kwa mishipa. Bila matibabu, ugonjwa wa moyamoya unaweza kusababisha kifo kwa sababu ya kuvuja damu ndani ya ubongo.

Matatizo yanayoweza kutokea

  • Kupooza

Vyanzo

https://medlineplus.gov/download/genetics/condition/moyamoya-disease.pdf

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi