UGONJWA WA PEPOPUNDA KWA WATOTO: Sababu, dalili, matibabu

Ugonjwa wa pepopunda kwa watoto wachanga ni nini?

Pepopunda ni ugonjwa wa hatari unaoambukiza.  Ugonjwa huu unasababishwa na vimelea vya bacteria vinavyoitwa “clostridium tetani”.  Vimelea hivi huingia mwilini kupitia kwenye kidonda au jeraha.  Ugonjwa huu huwapata watu wa rika zote.  Kwa watoto wachanga toka kuzaliwa hadi kufikia umri wa siku 28, vimelea huingia mwilini kupitia kwenye kitovu kilichokatwa kwa kutumia kifaa chenye maambukizi, kama vile wembe, mabua na usinge au kuwekwa vitu vichafu kama vile kinyesi cha ng’ombe, vumbi la kizingitini na kadhalika.

Dalili za ugonjwa wa pepopunda kwa watoto wachanga?Pepopunda

Mtoto mchanga aliyepatwa na pepopunda huwa na dalili zifuatazo ambazo hujitokeza siku mbili au tatu baada ya kuzaliwa.

Athari za ugonjwa wa pepopunda kwa watoto

Ugonjwa huu unaua katibu watoto wote wanaoupata

Kuzuia ugonjwa wa pepopunda kwa watoto

Ugonjwa huu huzuilika kwa chanjo ya Pepopunda. Ili kumkinga mtoto mchanga njia pekee ni kumpatia mama kinga kabla au wakati wa ujauzito. Kinga kamili hupatikana kwa dozi tano za sindano kwa ratiba ifuatavyo: –

Chanjo Muda Kinga
Chanjo ya kwanza Wakati wowote Hamna
Chanjo ya pili Wiki nne baada ya sindano ya kwanza Miaka mitatu
Chanjo ya tatu Miezi sita baada ya sindano pili Miaka mitano
Chanjo ya nne Mwaka mmoja baada ya sindano ya tatu Miaka 10
Chanjo ya tano Mwaka mmoja baada ya sindano ya nne Miaka 20

Ikithibitika kuwa mama aliwahi kupata chanjo tatu za DTP utotoni, itahesabiwa ameshapata dozi mbili za chanjo ya Pepopunda, hivyo itabidi aendelee na dozi zingine za chanjo ya Pepopunda ili kukamilisha ratiba.

Matibabu ya ugonjwa wa pepopunda kwa watoto

Ugonjwa wa pepopunda hauna tiba.

Ujumbe muhimu

  • Ni muhimu wanawake wote wenye umri wa kuzaa kati ya miaka 15 hadi 49 wapate chanjo kamili dhidi ya ugonjwa wa Pepopunda, ili kumkinga mtoto atakayezaliwa.
  • Zingatia usafi wakati wa kuzalisha, kukata na kutunza kitovu kuzuia maambukizi, kitovu cha mtoto kisiwekwe kitu chochote.
  • Mama atunza kadi yake ya chanjo ya Pepopunda kwa ajili ya kumbukumbu.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/000615.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi