Magonjwa ya ndani ya mwili

UGONJWA WA SURUA :Dalili, Sababu, Matibabu…

surua

Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko

Maelezo ya jumla

Surua ‘’measles’’ ni ugonjwa unaoweza kuambukizwa kwa urahisi sana, na ulikuwa ugonjwa uliowapata watoto wengi sana kabla ya enzi ya chanjo kuanza. Inaweza kuchukua mpaka siku 10 kabla ya dalili kuonekana baada ya kuambukizwa. Mwanzoni mtoto anapatwa na kikohozi kikavu, kuchuruzika makamasi, macho yakuwa mekundu na baadae homa. Baada ya siku 2 – 4, madoadoa mekundu au kahawia hujiokeza usoni na baadae kusambaa miguuni na mwili mzima. Kunaweza kuwepo madoa meupe kwenye sehemu ya ndani ya mashavu. Watoto wengi hupona vizuri tu. Lakini surua inaweza kusababisha maambukizi sikioni na matatizo mengine kama vile homa ya mapafu na kwa mara chache kuvimba ubongo.

Ukiwa na Surua mwone daktari;

Panga kumpeleka mtoto akaonwe na daktari ili atambue ugonjwa huu na kuanzisha matibabu yanayostahili

Unachoweza kufanya wewe mwenyewe ukiwa na Surua

Surua ni ugonjwa unaoleta karaha sana na wakati mwingine mtoto anaweza kuonekana mgonjwa sana. Unaweza kujaribu njia zifuatazo ili kupunguza karahasurua

  • Kama mtoto ana homa mpatie dawa za kupunguza maumivu ili kupunguza homa
    • Dawa kama vile ‘’actaminophen’’ au ‘’ibuprofen’’
    • Muulize mfamasia kupendekeza dawa itakayofaa kwa mtoto
  • Mvishe mtoto nguo nyepesi na weka ‘’fan’’ inayozunguka chumbani kwake
  • Mpatie mwanao maji ya kutosha wakati wote wa siku ili kurejesha maji yanayopotea kwenye jasho
  • Japo sio lazima mtoto abakie kitandani, ni muhimu akabakia kitandani mpaka homa itapoanza kushuka
  • Vinywaji vya moto viasadia kupunguza kikohozi
  • Punguza mwanga wa chumba kama mwanga unamuumiza macho
  • Hewa ya moto yenye unyevunyevu husidia kuzibua pua na njia ya mfumo wa hewa. Unaweza kuongeza mvuke chumbani kwa kuweka bakuli lenye maji karibu na ”radiator” au unaweza kumwogesha kwenye maji ya uvuguvugu
  • Mtoto atakuwa na uwezo wa kuambukiza wengine kwa muda wa siku 5 baada ya upele kuanza kuonekana. Baada ya hapa anaweza kuanza kwenda shule kama anajisikia vizuri na kama hakuna matatizo mengine yoote yaliyojiokeza

Kuzuia ugonjwa wa surua

Chanjo ya kuzia surua hutolewa katika chanjo inayoitwa MMR (Chanjo hii hukinga maginjwa matatu, Surua ‘’Measles’’, ‘’Mumps’’, ‘’rubella’’). Hakikisha kuwa mwanao amepata chanjo ya surua.
Angalia pia : Ratiba ya chanjo za watoto Tanzania

Mwone dakatari

Panga kumwina daktari haraka sana kama:

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001569.htm

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X