Magonjwa ya akili

UGONJWA WA USONJI: Sababu, dalili, matibabu

usonji

Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko

Usonji ni nini?

Usonji ni neno mwamvuli linalotumika kuelezea matatizo ya tabia na kushindwa kuwasiliana. Dalili za usonji zinaweza kuwa nyepesi, za kadri au kali sana.

Ni zipi dallili za usonji?

Dalili za usonji mara nyingi huanza kuonekana utotoni. Baadhi ya dalili na ishara huanza kuonekana kati ya miezi sita na 12 ya umri. Dalili zinazoonekana zaidi ni zile za tabia zisizo za kawaida na kuchelewa kuongea. Baadhi ya dalili na ishara muhimu ni pamoja na:

  • Kuchelewa kuongea ua kuchelewa kuanza kuwasiliana na wengine
  • Mjongeo wa mwili unaojirudia rudia – anaweza kufanya kitendo na kukirudia rudia rudia
  • Ana kuwa na vitu vichache anavyopenda kufanya
  • Hapendi kuwaangalia watu machoni au anafanya hivyo mara chache sana
  • Ni ngumu kwake kuelezea hisia zake au mapenzi yake
  • Anahangaika au kukasirishwa ukibadili mwenendo au shughuli zake za kila siku
  • Anashindwa kuanzisha au kuendeleza mazungumzo
  • Anakuwa na mapenzi makubwa na baadhi ya vitu – ukimnyang’anya anakasirika na kuwa mwenye vurugu
  • Anashtushwa sana na sauti au mwanga au vitu vya kuonekana
  • Haoneshi dhamira ya kutengeneza mrafiki – anapenda kubaki mwenyewe bila marafiki
  • Anashindwa kucheza na watoto wengine

Unaweza kudhani kuwa mtoto wako ana usonji kama ukiona tabia zifuatazo:

  • Hanyooshi kidole kukuonesha vitu anavyotaka
  • Hajibu chochote unapomuita jina lake
  • Haongei nawe – Hajibu unapomuuliza
  • Matendo yasiyo ya kawaida, kama vile kutembelea vidole vya miguu, ukung’uta viganja vya mikono, kuchunguza vitu kwa umakini huku amevisogeza karibu na uso au kwa kuviangalia kupitia kona ya jicho, au kuchezesha vidole isivyo kawaida karibu na jicho

Usonji unasababishwa na nini?

Hakuna sababu moja inayojulikana inayosababisha usonji. Kunaweza kuwepo na hatari ya kupata usonji kama kuna mtu kwenye familia ana usonji. Kama mama na baba wamepata mtoto katika umri mkubwa ni moja ya sababu zinazoongeza hatari ya mtoto kupata usonji. Kuna hatari kubwa pia ya kupata usonji kama mama ana ugonjwa wa kisukari, shinikizo la juu la damu, maambukizi, au kama anatumia baadhi ya dawa (kwa mfano valproate) au kama amekutana na dawa za kuulia wadudu.

Je, Chanjo zinaweza kusababisha ugonjwa huu?

Hapana, kuna tafiti nyingi kubwa zilizofanyika na zinaonesha chanjo ni salama na hazisababishai usonji

Usonji unatambuliwaje?

Watoto wenye usonji wanaweza kuwa na dalili na ishara zinazoshabihiana na wale wenye matatizo mengine, kama vile magonjwa ya akili. Kama wazazi au daktari anadhani kuwa mtoto ana usonji, anapaswa kufanyiwa uchunguzi na mtaalamu wa ugonjwa huu. Wakati mwingine linahitaika jopo la wataalamu ili kufanya utambuzi huu. Kwa watoto wenye dalili nyepesi za usonji, utambuzi unaweza kuwa mgumu sana.

usonjiUsonji unatibiwa vipi?

Hakuna dawa ya kutibu na kuponya kabisa usonji. Watoto wenye usonji wanabakia na dalili maisha yao yote. Moja ya matibabu ya kwanza ya ugonjwa huu ni ya kujenga tabia mapema – early intensive behavioral untervention. Hii inaweza kuanza mapema iwezekanavyo baada ya utambuzi. Moja ya njia ambayo imefanyiwa tafiti za kutosha inaitwa applied behavior analysis therapy. Hii imeoneka kuboresha uwezo wa kiakili, lugha, na mahusiano kama itatumiwa kwa muda mrefu.

Dawa zinapaswa kutumiwa pale tu kunapokuwepo na ugonjwa mwingine na tabia zinashindwa kudhibitiwa na tiba ya kurekebisha tabia. Dawa zinazotumika kutibu usonji zina madhara mabaya makubwa. Zinapaswa kutumiwa pale tu inapobidi, na kama faida zitakazoletwa zinazidi hatari iliyopo.

Wazazi wanaweza kusoma na kujifunza njia nyingi mbadala za kushughulikia usonji, lakini sio zote ni salama na thabiti. Melatonin imefanyiwa utafiti wa kutosha na inafaa kwa kutibu matatizo ya usingizi. Baadhi ya matibabu mengi hayajaonesha uwezo wa kudhibiti dalili za usonji. Kama ungependa kujaribu njia mbadala, ni vizuri kuongea na daktarin kwanza kabla ya kuzitumia.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/autismspectrumdisorder.html

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X