UGONJWA WA VON WILLEBRAND: Sababu, dalili, matibabu

Ugonjwa wa von Willebrand ni nini?

Ugonjwa unaofanana na ugonjwa wa hemophilia, unasababisha kuvuja damu. Ugonjwa wa von Willebrand unawapata watu wengi zaidi na hauna dalili kali sana ukiulinganisha na ugonjwa wa hemophilia. Kiambata cha protini kinachoitwa von Willebrand kinachopatikana kwenye damu, ni muhimu na kinahitajika ili kusaidia damu kuganda. Kwa watu wenye ugonjwa wa von Willebrand kiambata hiki hakifanyi kazi vizuri.

Kuna aina kuu tatu za ugonjwa wa von Willebrand. Aina ya 1 na ya 2 zina dalili nyepesi kidogo ukilinganisha na aina ya 3. Ugonjwa huu ni wa kurithi. Unaweza kupata aina ya 1 au ya 2 ya ugonjwa huu kama mzazi mmoja ana jeni za ugonjwa huu. Hata hivyo, unaweza kupata aina ya 3 pale tu wazazi wote wawili wanatakuwa na jeni za ugonjwa huu. Japokuwa ugonjwa wa von Willebrand unawapata zaidi wanafamilia, unaweza kuhusisha na aina kadhaa za matatizo ya kitabibu. Aina hii ya ugonjwa wa von Willebrand si ya kurithi.

Nitajuaje kama nina ugonjwa wa von Willebrand?ugonjwa wa von Willebrand

Inategemea una aina gani ya ugonjwa huu na una dalili kali kiasi gani. Unaweza kuona dalili zifuatazo, au unaweza usione dalili yoyote.

Dalili za ugonjwa wa von Willebrand ni pamoja na:

Kama una ugonjwa mkali wa von Willebrand:

  • Unaweza kuvuja damu bila sababu yoyote
  • Kupata maumivu na kuvimba viungo na misuli kwa sababu ya kuvuja damu
  • Kujaa kwa damu chini ya ngozi na kusababisha uvimbe au kuvia damu chini ya ngozi

Kama una dalili kadhaa kati ya hizi, daktari anaweza kuagiza ufanye vipimo kadhaa ili kutambua kama una ugonjwa wa von Willebrand au aina nyingine ya ugonjwa unaosababisha kuvuja kwa damu. Vipimo hivi husaidia kuangalia kama damu inaganda vizuri. Baadhi ya vipimo vinaweza kuhitajika kufanyika mara kadhaa ili kuhakikisha kuwa una ugonjwa wa von Willebrand.

Ugonjwa wa von Willebrand unatibiwa vipi?

Hakuna tiba ya kuponya kabisa ugonjwa wa von Willebrand, lakini unaweza kutumia dawa ili damu iweze kuganda vizuri zaidi. Kwa kawaida, unahitaji matibabu pale tu unapohitaji kufanyiwa upasuaji au kufanyiwa utaratibu wa kung’oa meno ili kuzuia damu kuvuja damu sana.

Unaweza kufanya yafuatayo ili kuzuia uvuja damu:

  • Epuka kutumia dawa zinazopunguza uwezo wa damu kuganda (kwa mfano dawa kama, aspirin na ibuprofen). Hakikisha unaongea na daktari kabla ya kutumia dawa.
  • Mwambie daktari au daktari wa meno kuwa una ugonjwa wa von Willebrand, kabla hajakupatia dawa au kukufanyia utaratibu wowote wa kitabibu.
  • Unaweza kuvaa kitambulisho kinachoonesha una ugonjwa wa von Willebrand ili kuwasaidia wataalamu wa afya kufahamu kuhusu ugonjwa wako utakapoumia na kupoteza fahamu.
  • Dhibiti uzito kwa mazoezi, kama vile kuogelea, kuendesha baiskeli, na kutembea. Epuka shughuli zinazohusisha kugongana au kuanguka, kama vile mpira wa miguu, hocket, mieleka, na kunyanyua vyuma vizito. Ongea na daktari kabla haujaanza kufanya mazoezi yoyote.

Wanawake wanapaswa kufahamu nini kuhusu ugonjwa wa von Willebrand?Ugonjwa wa von Willebrand

Kupata hedhi nzito ndio dalili kuu kwa wanawake wenye ugonjwa wa von Willebrand. Unapata damu nzito kama unapata mabonge makubwa zaidi ya sentimeta 2 kwa upana wakati wa hedhi. Unaweza kuhitajika kubadili taulo yako ya kike (pad/tampon) mara kadhaa ndani ya saa moja, hasa kama utakuwa na kiwango kidogo cha madini ya chuma (upungufu wa damu). Kuna sababu nyingine za kupata hedhi nzito, kwa hiyo, daktari atahitaji kutofautisha kabla hajakupima kama una ugonjwa wa von Willebrand.

Baadhi ya njia za kupanga uzazi zinawea kusaidia kupunguza kiwango cha damu unayopata wakati wa hedhi. Baadhi ya wanawake wanachangua kufanyiwa upasuaji ili kuondoa kabisa mfuko wa uzazi kama hawana mpango wa kupata watoto hapo baadae.

Ujauzito unaweza kuwa ngumu kwa wanawake wenye ugonjwa wa von Willebrand kwa sababu wanavuja damu sana wakati na baada ya kujifungua. Hata hivyo, wanawake wengi wenye ugonjwa huu wanapata ujauzito na kupata mtoto bila matatizo. Utapata vipimo wakati wa ujauzito, na unaweza kuhitaji dawa ili kudhibiti kuvuja damu wakati wa kujifungua. Daktari aliyebobea katika kusaidia wanawake wenye ujauzito ulio hatari atasaidia kukuongeza katika kipindi chote cha ujauzito na kujifungua.

Angalizo

Maelezo haya yanatoa muhtasari kuhusu ugonjwa huu kwa makusudi ya kuelimisha na kutoa habari na unaweza usimfae kila mtu. Ongea na daktari kupata habari zaidi zinazokuhusu wewe kabla ya kufanya maamuzi yoyote ya kitabibu.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/000544.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi