UGONJWA WA WILSON: Sababu, dalili, matibabu

Maelezo ya jumla

Ugonjwa wa wilson (Wilson’s disease) ni tatizo la kurithi linalosababisha kubakia kwa kiwango kikubwa cha madini ya shaba kwenye tishu za mwili. Kiwango kikubwa cha madini ya shaba ndani ya mwili husababisha uharibifu wa ini na mfumo wa fahamu.

Ni zipi dalili za ugonjwa wa Wilson?ugonjwa wa wilson

Zifuatazo ni dalili za ugonjwa wa wilson:

 • Mkao usio wa kawaida wa mikono na miguu
 • Kuchanganyikiwa au kutokujielewa
 • Ugonjwa wa dementia
 • Kupata shida/ugumu kujongesha mikono na miguu, kukaza kwa misuli
 • Kupata shida/ugumu kutembea
 • Mabadiliko ya tabia au hisia
 • Mabadiliko ya hulka ya mtu
 • Woga, kujihisi kutokujiami
 • Kujongea taratibu
 • Kupungua kwa kujongea kwa misuli ya uso
 • Kupata shida kuongea
 • Mikono inaanza kutetemeka au viganja vya mikono
 • Mjongeo asioweza kuudhibiti – mgonjwa anaweza kushtuka bila kujijua
 • Kutapika damu
 • Uchovu
 • Ngozi kubadilika na kuwa ya njano au sehemu nyeupe ya jicho kuwa ya njano

Nani yuko kwenye hatari zaidi?

 • Ugonjwa wa wilson ni tatizo adimu sana la kurithi. Kama wazazi wote wana jeni mbaya zinazosababisha ugonjwa wa wilson, kuna 25% kwa kila ujauzito kuwa mtoto anaweza kupata tatizo hili.
 • Ugonjwa wa wilson unasababisha mwili kufyonza kiwango kikubwa cha shaba na kukibakiza mwilini. Kiasi hiki cha shaba kinarundikana kwenye ini, ubongo, figo, na macho. Mrundikano wa shaba unaweza kusbabisha kuharibika kwa tishu, kuzifanya tishu kufa kabisa, na kusababisha makovu ambayo husababisha kiungo kilichoathirika kushindwa kufanya kazi.
 • Ugonjwa huu mara nyingi unawapata zaidi watu wa ulaya mashariki, sicilia, na watu wa kusini mwa italia, lakini watu wengine wanaweza kuupata pia.
 • Ugonjwa wa wilson kwa kawaida unawapata zaidi watu wenye umri chini ya miaka 40. Kwa watoto, dalili huanza kuonekana katika mwaka wa 4 wa umri.

Utambuziugonjwa wa wilson

Kipimo cha kuchunguza macho kinachoitwa “slit-lamp” hufanyika ili kuonesha:

 • Kama mjongeo wa macho uko sawa
 • Kama kuna mviringo wenye rangi kama ya kutu kuzunguka iris ya jicho – kayser-fleischer rings

Uchunguzi wa mwili unaweza kuonesha ishara kama:

Vipimo vya maabara vitajumuisha:

 • Vipimo kuangalia kiwango cha seli zilizo kwenye damu – CBC
 • Kupima kiwang cha ceruloplasmin – protini hii hufanya kazi ya kutunza na kubeba shaba kutoka kwney ini kwenda kwenye damu na kuipeleka mwili mzima
 • Kupima kiwango cha shaba kwenye damu
 • Kupima kiwango cha asidi ya uric kwenye damu – kiwango cha asidi hii kikiongezeka humaanisha figo hazifanyi kazi vizuri ya kuiondoa mwilini
 • Kupima kiwango cha madini ya shaba kwenye mkojo

Kama kuna matatizo ya ini, vipimo vya maabara vinaweza kukuta:

 • Kiwango cha juu cha AST na ALT
 • Kiwango cha juu cha bilirubin
 • Kiwango cha juu cha PT na Aptt
 • Kiwango cha chini cha Albumin

Vipimo vingine ni pamoja na:

 • Kupima kiwango cha shaba kwenye mkojo kwa masaa 24
 • Picha ya eksirei ya tumbo
 • Picha ya MRI ya tumbo
 • Picha ya CT scan ya tumbo
 • Picha ya CT scan ya kichwa
 • Picha ya MRI ya kichwa
 • Kuchukua sampuli kwenye ini kwa ajili ya kuipima kwa darubini – biopsy

Ni wakati gani unapaswa kutafuta msaada wa kitabibu?

Ongea na dakatari kama una dalili yoyote ya ugonjwa wa wilson. Kama una historia kwenye familia ya kuwepo mgonjwa mwenye ugonjwa wa wilson, ni vizuri kuonana na mtaalamu wa maswala ya jeni wakati unapanga kupata mtoto.

Uchaguzi wa mataibabu

Lengo la matibabu ni kupunguza kiwango cha shaba kwenye tishu za mwili. Hili linafanyika kwa kufanya utaratibu unaoitwa “chelation” – unapatiwa dawa inayoweza kujishikiza kwenye shaba na kuiongoza kutoka nje kupitia kwenye kinyesi au mkojo. Matibabu haya yanaendea katika kipindi chote cha maisha yake.

Dawa zifuatazo zinaweza kutumika:

 • Penicillamine – hii hujishikiza kwa shaba na kuongeza kiwango cha shaba kinachotoka kwenye mkojo
 • Trientine – hii hujishikiza kwa shaba na kuongeza kiwango cha shaba kinachotoka kupitia mkojo
 • Zinc actate – hii huzuia shaba isifyonzwe nyingi tumboni au kwenye utumbo
 • Vitamin E inaweza pia kutumika.

Wakati mwingine, dawa zinazotumika kusaidia kuondoa shaba zinaweza kusababisha athari kwenye ubongo na mfumo wa fahamu.

Mlo ulio na kiwango kidogo cha shaba kinashauriwa. Baadhi ya vyakula unavyopaswa kuepuka ni pamoja na:

 • Chocolate
 • Matunda yaliyokaushwa
 • Ini
 • Uyoga
 • Karanga

Unaweza pia kuhitaji kunywa maji ya chupa/kisima, kwa sababu, mara nyingi maji ya bomba yanapita katika mabomba yaliyotengenezwa kwa saba. Epuka kutumia vyombo vya kupikia vilivyotengenezwa kwa shaba.

Dalili zinaweza kutibiwa kwa mazoezi. Watu ambao wanaonekana kuchanganyikiwa na hawawezi kujihudumia wenyewe, wanaweza kuhitaji msaada zaidi.

Kupandikiza ini jingine inweza kuhitajika kama ini la mgonjwa limeharibika sana.

Mtarajio

Utaendelea kupata matibabu maisha yako yote ili kudhibiti ugonjwa wa wilson. Ugonjwa huu unaweza kusababisha matatizo makubwa na hata kifo, kwa mfano, kuharibika kabisa kwa ini na uharibia mfumo wa fahamu unaosababishwa na shaba. Kama ugonjwa wa wilson usipokuua, dalili zinaweza kukufedhehesha.

Matatizo yanayoweza kutokea

Yafuatayo ni baadhi ya matatizo yanayoweza kukupata ukiwa na ugonjwa wa wilson:

 • Upungufu wa damu
 • Matatizo yanayotokana na kuharibika kwa mfumo wa fahamu
 • Kuharibika kwa ini/sirosisi
 • Kufa kwa tishu za ini
 • Kuwa na ini lililojaa mafuta – halifanyi kazi vizuri
 • Homa ya ini
 • Kuongezeka kwa uwezekano wa kuvunjika mfupa
 • Kuongezeka kwa uwezekano wa kupata maambukizi
 • Majeraha kwa sababu ya kuanguka
 • Manjano
 • Kukakamaa na ulemavu wa viungo
 • Kupoteza uwezo wa kujihudumia
 • Kupoteza uwezo wa kufanya kazi nyimbani na kazini
 • Kupoteza uwezo wa kushirikiana na wengine
 • Matatizo ya kisaikolojia
 • Matatizo ya badama

Kuharika na kushindwa kwa ini kufanya kazi na uharibifu wa mfumo wa fahamu (ubongo, uti wa mgongo) ndi matatizo hatari zaidi yanayowapata wagonjwa wengi wa ugonjwa wa Wilson. Ugonjwa wa Wilson unaua.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/wilsondisease.html

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi