Magonjwa ya wanawake

Uhusiano wa VVU/UKIMWI na UJAUZITO/MIMBA

ujauzito na ukimwi

Last Updated on October 12, 2023 by Dr Mniko

Je, watu walioambukizwa VVU wanaweza kupata au kuzaa watoto ambao hawana virusi?

Ndio.

  • Hii ni mojawapo ya faida nyingi za matibabu ya VVU (tumia dawa za kupunguza makali ya VVU/ART).
  • Unaweza kupata watoto ukiwa umeadhirika na VVU.
  • Tafadhali zungumza na daktari wako ikiwa umeamua kuwa mjamzito.
  • Katika nchi ya Tanzania, watu wanaoishi na VVU wanapaswa kupokea huduma na msaada sawa na watu wasio na VVU.
  • Hii ni pamoja na huduma ya kukusaidia kuwa mjamzito
  • Dawa za kufubaza virusi vya  ukimwi (ART) zinamlinda mshirika wakati wa utungaji wa mimba ikiwa mwenziwe ana VVU
  • ART zinamlinda mtoto dhidi ya VVU wakati wa ujauzito na wakati wa kuzaliwa

Kupanga ujauzito wako ukiwa na VVU/Ukimwiujauzito na ukimwi

Kupanga kupata ujauzito hakuna tofauti yoyote kama wewe ni mwaathirika wa VVU au sio mwathirika.

Lakini ikiwa hivi karibuni imethibitishwa kua umeambukizwa VVU wakati wa ujauzito, kuna uwezekano unastahili msaada zaidi.

Ikiwa tayari una VVU, daktari anaweza kukuhudumia afya yako kabla hujapata ujauzito – na pia kukuchunguza kwa makini na kuufuatilia ujauzito wako.

Chagua wanahuduma wa afya pamoja na zahanati ya ujauzito ambayo inakupa usaidizi na inayouheshimu uamuzi wako wa kutaka kupata mtoto.

Kwa watu wengi, kupata ujauzito kwa kutumia njia ya kawaida ndio chaguo la kwanza. (kiwango cha chembechembe za VVU katika damu ya muathirika inajulikana kwa lugha ya Kiingereza kama “HIV Viral Load”). Ikiwa imethibitishwa ya kwamba muathirika wa VVU ana kiwango cha chini cha idadi ya VVU mwilini, basi utumizi wa ART utazuia kuambukiza mwenzi ambaye hana VVU.

Hii idadi ndogo ya chembechembe za VVU inapaswa kwanza kuthibitishwa kwa miezi kadhaa kabla ya kuamua kusitisha matumizi ya kondomu.

Kuamua kupata ujauzito kwa kutumia ile njia ya kawaida ni jambo ambalo washirika wote wawili wanastahili kulijadili na kukubaliana.

Daktari wako anaweza kukuelimisha uelewe lini unapoweza kupata mimba kulingana hasa na mzunguko wako wa hedhi.

Je, dawa za kufubaza virusi (ART) ni salama kwa mama?

Ndio.

  • Maelfu ya tafiti za mimba unathibitisha ya kwamba hakuna madhara yoyote makubwa kwa mtoto kutokana na matumizi ya ART.

Je, dawa za kufubaza virusi (ART) ni salama kwa mtoto?

Ndio.

  • Maelfu ya tafiti za mimba unathibitisha ya kwamba hakuna madhara yoyote makubwa kwa mtoto kutokana na matumizi ya ART.

Nitajifungua kwa njia ipi nikiwa na ujazito na VVU?

Ikiwa kiwango cha VVU mwilini mwa mama ni kidogo mpaka hakionekani kwa kipimo baada ya matumizi ya ART ndani ya wiki 36, miongozo ya Tanzania inapendekeza kujifungua kwa kutumia njia ya kawaida ya uke. Katika hali nyingine upasuaji uliyopangwa unapendekezwa, hasa wakati wa dharura.

Kulinda na kuhakikisha afya ya mama

Afya yako mwenyewe na matibabu yako ni mambo muhimu zaidi ya kuzingatia ili kuhakikisha unajifungua salama na kupata mtoto mwenye afya. Hili ndilo jambo la muhimu zaidi.

Kuzingatia na kufuatilia kumeza dawa ni muhimu

Kuzingatia na kufuatilia kumeza dawa ya ART kama ulivyoshauriwa na daktari ni muhimu sana. Kuchelewachelewa kumeza dawa kunapunguza ufanisi wa dawa hadi kiwango ambacho makali yanapungua. Kamwe usizidishe kipimo cha dawa hata kama umesahau kumeza/kutumia kipimo kimoja au dozi moja.

Kumlisha mtoto wako baada ya kujifungaumtoto

Wanawake ambao wameambukizwa VVU au ambao wana UKIMWI wanaweza kutumia njia ya kunyonyesha. Kunyonyesha maziwa ya mama hakutafanya hali yao iwe mbaya. Hata hivyo, kuna uwezekano wa mama mwenye VVU kumwambukiza mtoto wake VVU kupitia kunyonyesha maziwa ya mama.

Kwa kuwa kwa ujumla watu wengi hunyonyesha, watoto 10 – 20 kati ya kila 100 wanaonyonya maziwa ya mama wataambukizwa VVU kupitia maziwa ya mama kujazia wale walioambukizwa wakati wa mimba na wakati wa kuzaliwa. Maambukizi ya VVU kupitia maziwa ya mama yanawezekana kwa kinamama waliozidiwa na ugonjwa au walioambukizwa karibuni.

Wanawake wanaomeza dawa za kupunguza makali ya UKIMWI wanaweza kutumia njia ya kunyonyesha. Ukweli, dawa ya kupunguza makali ya UKIMWI katika wiki za mwanzo za kunyonyesha maziwa ya mama zinaweza kupunguza hatari ya maambukizo ya VVU kupitia maziwa ya mama.

Kumpatia mtoto lishe mbadala hakuna hatari ya maambukizi ya VVU. Na hili linaruhusiwa pale tu kama tu chakula mbadala kitafaa, kinapatikana, nafuu, endelevu, na salama, kinapendekezwa kwa miezi 6 ya mwanzo baada ya mtoto kuzaliwa. Iwapo chakula mbadala kilichopo hakiwezi kukidhi vigezo hivi 5, kumnyonyesha maziwa ya mama pekee kwa miezi 6 ya mwanzo ndiyo njia salama zaidi ya kumlisha mtoto.

Mkakati mmoja wa kufanya unyonyeshaji maziwa ya mama uwe salama ni kukamua maziwa ya mama na kuyapasha moto.

Wahimize wanawake wenye VVU watumie kondomu pamoja na njia ya kunyonyesha. Zikitumiwa wakati wote na kwa usahihi, kondomu husaidia kuzuia maambukizi ya VVU na magonjwa mengine ya ngono.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/hivaidsandpregnancy.html

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X