Msaada wa Haraka! 255 759 07 960
Kwa Kina
Tafuta
 1. Home
 2. UKURUTU

UKURUTU

 • August 19, 2020
 • 0 pendwa
 • 33 Wameona
 • 0 Maoni

Maelezo ya jumla

Ukurutu (eczema) , ni neno linalotumika kuwakilisha aina mbalimbali za uvimbe wa ngozi. Ukurutu hujulikana pia kama ugonjwa wa ngozi (dermatitis). Ukurutu sio hatari, lakini aina nyingi za ukurutu husababisha ngozi kuwa nyekundu, kuvimba na kuwasha. Mambo ambayo yanaweza kusababisha ukurutu ni pamoja na magonjwa, vitu vinavyowasha, mzio (allergy)  na muundo wa kijenetiki. Ukurutu hauambukizwi.

Aina ya ukurutu inayowapata watu wengi ni atopic dermatitis. Hii ni hali ya mzio ambayo hufanya ngozi kuwa kavu na kuwasha. Inawatokea zaidi watoto wachanga na watoto wakubwa.

Ukurutu hauwezi kuponywa, lakini mtu anaweza kuzuia aina fulani za ukurutu kwa kuepuka kukutana na vitu vinavyowasha,msongo wa mawazo na vichochezi vya mzio.

Je,ni nini dalili za ukurutu ?

Ukurutu si ugonjwa mmoja,kuna aina nyingi za ukurutu na kila aina huonesha mkusanyiko wa dalili nyingi tofauti. Kuvimba kwa ngozi ni dalili inayopatika katika aina zote za ukurutu. Zifuatazo ni dalili za aina kadhaa za ukurutu

 • Atopic Eczema -hii ndio aina ya ukurutu inayowapata watu wengi zaidi, inafikiriwa kuwa aina hii ya ukurutu ina uhusiano wa kijenetiki na pumu. Mzio husababisha ukurutu kutokea sehemu yoyote ya mwili hata kama sehemu hiyo haijagusana na kizio (Kizio -(allergen) ni kitu chochote kinachochochea kutokea kwa mzio). Vipele vinavyowashawa hutokea hasa kichwani, shingoni, sehemu ya ndani ya kiwiko.sehemu ya nyuma ya magoti na kwenye matako.
 • Contact dermatitis¬≠- hii ni aina ya ukurutu inayotokea baada ya kugusa kizio au kitu chochote kinachoweza kusababisha harara,kwa mfano mgonjwa anayetumia kemikali kusafishia nyumba anaweza kupata ukurutu baadae, mikono yake inaweza kupata vipele na kuwasha na hata kuchubuka.
 • Eczema Xerotic – Ngozi ya mgonjwa huwa kavu sana na kupasuka pasuka ,baadae hutengeneza vipele. Mara nyingi hali hii huwapata zaidi wazee
 • Seborrhoeic dermatitis –  Ngozi ya kichwa, kope, uso na kiwiliwili huanza kubanduka , ngozi ya sehemu hizi inaweza kuwa kavu au yenye mafutamafuta.

Uchaguzi wa matibabu

Hakuna tiba ya kukuponya kabisa ukurutu, lakini kuna matibabu kadhaa yanayopunguza uvimbe na kuwasha:   

 • Corticosteroids:-dawa hizi zinatofautiana, kuna ambazo zina nguvu kuliko zingine ,na daktari huzitoa kulingana na ukali wa ugonjwa wako. Dawa hizi zikitumiwa kwa muda mrefu zinaweza kuwa na madhara, kama vile; kusababisha ngozi kuwa nyembamba sana na kusababisha maambukizi kwenye ngozi. Dawa hizi hazipendekezwi kutumika kama kinga.
 • Mafuta ya kukinga ngozi- mafuta haya yanayotengenezwa kwa ceramides, free fatty acids na lehemu hunuia kurekebisha ngozi iliyoharibika.
 • Immunomodulators:-hupunguza mfumo wa kinga katika maeneo yaliyoathirika. Dawa hizi mara nyingi hutumiwa zaidi katika hali kali sana za ukurutu, hii ni kwa sababu zinafikiriwa kuwa zinaweza kuchangia kutokea kwa saratani ya tezi za limfu au ngozi.
 • Antibiotics -kwa maambukizi yoyote yanayotokea baada ya ngozi kuharibiwa na ukurutu.
 • Dawa za kupunguza kuwashwa

Magonjwa yenye dalili zinazofanana na ukurutu

Kwa sababu ukurutu wakati mwingine husababishwa na chakula, mara nyingi watu huchanganya mzio wa chakula na ukurutu.

Kuzuia ukurutu    

 • Watu wenye ukurutu, au watu wanaoishi na mtu aliye na ukurutu, ambao hawako katika hatari ya ya kupata ndui (smallpox), inashauriwa wasipewe chanjo ya ndui kwa sababu inaweza kusababisha vidonda vya chanjo.    
 • Ongeza unyevunyevu kwenye ngozi. Epuka kutumia sabuni na madawa makali.    
 • Hatua za kimazingira, kama vile kuepuka vumbi.     .    
 • Mlo, Wagonjwa wanapaswa kuepuka aina ya chakula fulani kinachochochea kutokea kwa ukurutu.

Vyanzo    

https://medlineplus.gov/eczema.html

 • Shirikisha:

Leave Your Comment