ULEVI

ULEVI

 • October 25, 2020
 • 0 Likes
 • 155 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Ulevi (Alcoholism) na unywaji wa pombe kupita kiasi (Alcohol abuse) ni matatizo mawili tofauti.

 • Ulevi ni pale unapopata dalili za kimwili za uraibu wa pombe lakini ukaendelea kunywa pombe, japo utapata matatizo ya kiafya, kiakili, kijamii, kifamilia na hata kazini,utaendelea kunywa. Pombe inaweza kutawala maisha na mahusiano yako.
 • Unywaji wa pombe kupita kiasi ni pale unywaji wako unapokusababishia matatizo, lakini haukusababishii utegemizi wa pombe.

Angalia pia unachoweza kufanya ukijisikia vibaya baada ya kunya pombe | Hangover

Ni nini dalili za ulevi?

 • Watu ambao ni walevi au wanaokunywa pombe kupita kiasi mara nyingi:
  • Huendelea kunywa, hata baada ya afya, kazi, au familia kuharibika kwa sababu ya pombe
  • Hunywa wakiwa peke yao
  • Huwa wagomvi/wenye vurugu wakati wa kunywa
  • Huwa wakali sana wakiulizwa kuhusu unwaji wao
  • Hawawezi kudhibiti unywaji: hawawezi kuacha au kupunguza kiasi cha pombe wanachokunywa
  • Huwa na visingizio vingi vya kunywa
  • Huwa watoro kazini au shuleni, au utendaji wao wa kazi hupungua kwa sababu ya kunywa
  • Huacha kushiriki katika shughuli kwa sababu ya pombe
  • Wanahitaji kutumia pombe ili siku iende,bila pombe siku inaharibika kabisa
  • Wanajisahau kula au wanakula vibaya
  • Wanapuuzia kuvaa vizuri na hawajali usafi
  • Hujaribu kuficha matumizi yao ya pombe
  • Hutetemeka asubuhi au baada ya kukaa muda kidogo bila kunywa
 • Dalili za utegemezi wa pombe ni pamoja na:
  • Kupoteza kumbukumbu baada ya kunywa sana
  • Huhitaji pombe nyingi zaidi na zaidi ili kulewa
  • Hujisikia vibaya baada ya pombe kuisha mwilini,au kama haujanywa kwa muda fulani
  • Kupata matatizo yanayohusiana na pombe kama vile ugonjwa wa ini wa unaosababishwa na pombe

Ni nini husababisha ulevi?

 • Hakuna sababu inayojulikana inayosababisha mtu kuwa mlevi au kutumia vibaya pombe. Utafiti unaonyesha kuwa jeni fulani zinaweza kuongeza hatari ya kuwa mlevi, lakini ni jeni gani na jinsi zinavyofanya kazi haijulikani.
 • Kiasi unachokunywa kinaathiri uwezekano wako wa kuwa mtegemezi wa pombe
 • Walio katika hatari ya ku walevi ni pamoja na:
  • Wanaume wanaokunywa vinywaji 15 au zaidi kwa wiki
  • Wanawake wanaokunywa vinywaji 12 au zaidi kwa wiki
  • Mtu yeyote ambaye anakunywa vinywaji vitano au zaidi kwa tukio angalau mara moja kwa wiki
  • Kinywaji kimoja kinaelezewa kama chupa yenye aunsi 12 za bia, Aunsi 5 za glasi ya mvinyo.
  • Uko kwenye hatari kubwa ya kutumia vibaya pombe na kuwa mtegemezi wa pombe kama una mzazi mlevi.
 • Unaweza pia kuwa katika uwezekano mkubwa wa kutumia pombe vibaya au kuwa mtegemezi wa pombe kama:
  • Ni kijana mdogo uliye kwenye shinikizo rika
  • Mwenye sonona,mwenye wasiwasi au skizofrenia
  • Kama upatikanaji wa pombe ni rahisi
  • Kama hajiamini
  • Kama ana matatizo ya kimahusiano
  • Anaishi maisha ya shida au yenye msongo mkubwa
  • Unaishi katika jamii ambayo utamaduni wa kutumia pombe ni wa kawaida na unakubalika
  • Matumizi mabaya ya pombe yanaongezeka. Karibu mtu 1 kati ya 6 nchini Marekani wana tatizo la unywaji wa pombe.

Wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Tafuta huduma ya matibabu ya haraka iwapo: Wewe au mtu unayemjua mwenye utegemezi wa pombe, anaonekana kuchanganyikiwa, anapata degedege au kutokwa damu

Utambuzi

 • Mtoa huduma wa afya atafanya uchunguzi wa mwili na kuuliza maswali kuhusu historia yako na familia, hii ni pamoja na matumizi yako ya pombe.
 • Maswali yafuatayo yanatumiwa na Taasisi ya Taifa ya Unywaji wa Pombe na Ulevi,ili kutambua matumizi mabaya au utegemezi wa pombe:
  • Je! Umewahi kuendesha gari ukiwa umekunywa?
  • Je! Unapaswa kunywa zaidi kuliko kawaida ili kulewa?
  • Je! Umewahi kuhisi kwamba unapaswa kupunguza unywaji wako?
  • Je, umewahi kupoteza fahamu na usikumbuke chochote baada ya kunywa?
  • Je! Umewahi kukosa kazini au kupoteza kazi kwa sababu ya unywaji?
  • Je, kuna mtu katika familia yako mwenye wasiwasi kuhusu unywaji wako?
  • Vipimo vinavyoweza kufanyika ni pamoja na:
   • Kupima kiasi cha pombe kwenye damu (hii inaweza kueleza kama mtu ametoka kunywa hivi karibuni, lakini hakiwezi kuthibitisha ulevi)
   • Complete blood count (CBC)

Uchaguzi wa matibabu

 • Kuacha kabisa matumizi ya pombe ndio lengo kuu la matibabu. Hii inaitwa kujizuia (abstinence).
 • Ushirika wa jamii na familia ni muhimu sana ili kufikia lengo hili.
 • Kuacha kabisa na kuepuka pombe ni jambo gumu kwa watu wengi. Kutakuwa na wakati mgumu. Unapaswa kuepuka kunywa pombe kwa kadri iwezekanavyo.
 • Watu wengine wanaotumia pombe vibaya  huweza kupunguza kiasi wanachokunywa. Hii inaitwa kunywa kwa kiasi (drinking in moderation). Ikiwa mbinu hii haitafanikiwa, unapaswa kujaribu kuacha kabisa kunywa.
 • Kipimo cha kupima kazi ya ini (Liver function tests)

KUAMUA KUACHA KUNYWA:

 • Watu wengi wenye matatizo ya pombe hawatambui kuwa wana matatizo.
 • Njia bora ya matibabu ni kumsaidia mtu kutambua ni kwa kiasi gani matumizi ya pombe hudhuru maisha yake na wale walio karibu yake.
 • Uchunguzi unaonesha kwamba, watu wengi wenye shida ya pombe, huchagua kuanza matibabu baada ya wanafamilia au waajiri kuwa wazi na kuwaambia kuhusu madhara yanayosababishwa na unywaji wao.
 • Kuacha pombe, ni bora kukafanyika katika mazingira ya udhibiti na usimamizi. Matatizo yanayotokana na kuacha pombe yanaweza kutishia maisha.
 • Mtoa huduma wa afya anapaswa kuagiza uchunguzi wa damu na mkojo ili kuangalia matatizo ya kiafya ambayo ni ya kawaida kwa watu wanaotumia pombe.

MSAADA WA MUDA MREFU:

 • Unaweza kusaidiwa kuacha kunywa pombe kabisa katika kituo cha kutibu utegemezi/uraibu wa pombe,kwenye vituo hivi mambo yafuatayo yanaweza kufanyika:
  • Ushauri na kujadilina kuhusu athari za ulevi na jinsi ya kudhibiti mawazo yako na tabia .
  • Msaada wa afya ya kiakili
  • Huduma ya matibabu
  • Unaweza kulazwa katika kituo maalum,kama mgonjwa wa ndani, au unaweza kuhudhuria katika programu kama mgonjwa wa nje.
  • Wakati fulani unaweza kupewa dawa ili kukuzuia kunywa tena.
  • Acamprosate – watu wanaoitumia dawa hii hupunguza maradufu uwezekano wa kurudia tena utegemezi wa pombe.
  • Disulfiram – Mtu anayetumia dawa hii hupata madhara mabaya sana (kutapika,kichefuchefu,kichwa kuuma n.k) hata baada ya kunywa kiasi kidogo tu cha pombe ndani ya wiki 2 baada ya kuitumia.
  • Naltrexone -inapunguza tamaa za pombe. Inapatikana kama sindano.
 • Huwezi kutumia dawa hizi kama ni mjamzito au una ugonjwa fulani. Dawa hizi mara nyingi hutumiwa sambamba na ushauri au msaada wa kitabibu.
 • Sonona au kuwa na wasiwasi uliopitiliza ni hali zinazoweza kutokea baada ya kuacha kutumia pombe. Matatizo haya yanapaswa kutibiwa mara moja.

Nini cha kutarajia ?

 • Kutengamaa kwa maisha ya mlevi hutegemea kama ataweza kuacha kunywa pombe.
 • Ulevi ni tatizo kubwa la kijamii, kiuchumi, na umma. Tatizo la kunywa linaweza kuathiri kila nyanja ya maisha ya mtu. Kam una tatizo la pombe, kujizuia kunaweza kusaidia kuboresha afya yako ya akili na kimwili na labda, hata mahusiano yako.
 • Usaidizi wa kimatibabu unaotolewa katika vituo vya uraibu yanaweza kukusaidia kuacha. Hata hivyo, kurudia tena kunywa baada ya matibabu ni jambo linalowezekan. Ni muhimu kuwa na watu wanaokusaidia na kukutia moyo.

Matatizo yanayoweza kutokea

 • Unywaji mbaya wa pombe, huongeza hatari ya kupata matatizo mengi ya kiafya, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuvuja damu tumboni
  • Uharibifu wa seli za ubongo
  • Ugonjwa wa ubongo unaitwa Wernicke-Korsakoff syndrome
  • Saratani ya koo, ini, koloni, na maeneo mengine
  • Mabadiliko kweny mzunguko wa hedhi
  • Delirium tremens –hii ni hali inayowatokea walevi wakikosa pombe kwa muda mrefu ,huweweseka,kuwa na wasiwasi mwingi,kuona vitu na kusikia sauti ambazo watu wengine hawazisikii na kuchanganyikiwa.
  • Ugonjwa wa kusahausahau (dementia) na kupoteza kumbukumbu
  • Sonona na kujiua
  • Kupungua kwa nguvu za kiume
  • Uharibifu wa moyo
  • Shinikizo la juu la damu
  • Kuvimba kwa kongosho (pancreatitis)
  • Ugonjwa wa ini
  • Uharibifu wa neva
  • Lishe duni
  • Matatizo ya kukosa usingizi (insomnia)
  • Matumizi ya pombe pia huongeza hatari ya kupata magonjwa ya zinaa.
  • Kunywa pombe wakati wa ujauzito kunaweza kusababisha mtoto kuzaliwa na kasoro .

Kuzuia

 • Taasisi ya Taifa ya Unywaji mbaya wa Pombe na Ulevi inapendekeza:
  • Wanawake hawapaswi kunywa zaidi ya kinywaji 1 kwa siku
  • Wanaume hawapaswi kunywa zaidi ya vinywaji 2 kwa siku
  • Kinywaji kimoja kinatajwa kama aunsi12 ya bia, aunsi 5 ya divai.
 • Vikundi vya msaada (Support groups)
  • Makundi ya msaada hayapatikani sana katika nchi zetu za kiafrika,nchi nyingi Afrika hazijalitambua vyema tatizo hili na kulitilia mkazo kama matatizo mengiene. Ila katika kituo cha hospitali utakachochagua kupata matibabu naamni vitakuwepo vikundi vya msaada. Usione aibu uliza,watu wanaopitia hali kama yako ni

Chanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/000944.htm

 

Leave Your Comment