UMUHIMU WA CHANJO: Majibu ya maswali yako

Mambo ya msingi

Chanjo ni Nini?

Chanjo huzuia mtu mwenye afya asipate magonjwa fulani kwa kufundisha mwili jinsi ya kutambua na kupambana nayo. Kwa kawaida huwa dawa ya sindano, matone au tembe kwa ajili ya kumeza.

Kwa nini chanjo ni muhimu?

Kuhakikisha kwamba familia inapokea chanjo zote ndio njia nzuri ya kuhakikisha afya yao. Chanjo ni njia nzuri za kuzuia magonjwa mengi hatari. Watoto wadogo wanaweza kupata magonjwa kwa sababu miili yao haijakomaa kupambana na magonjwa, kwa hivyo ni muhimu umpe mtoto chanjo haraka iwezeikanavyo.

Ninafaa kumpa mtoto wangu chanjo lini?

Chanjo ya homa ya manjano
Pata chanjo kujikinga

Madaktari wanapendekeza kwamba watoto wapokee chanjo tofauti wakiwa na umri fulani. Chanjo zingine pia zinahitaji zaidi ya dozi moja ili zifanye kazi. Kama ungependa kujua RATIBA YA CHAJO KWA WATOTO NCHINI TANZANIA bonyeza HAPA.

Mimi na familia yangu tunaweza kupata chanjo wapi?

Unaweza kupata chanjo katika kituo kilicho karibu na wewe. Zungumza na daktari ili kutambua mwanao anahitaji aina gani ya chanjo.

Chanjo inagharimu kiasi gani cha pesa?

Chanjo za watoto ni bure na zinatolewa katika mpango wa chanjo wa taifa kwa watoto wote. Mpleke mtoto katika kituo kilicho karibu yako.

Maswali na wasiwasi wa kawaida

Mtoto wangu hajapokea chanjo zote zinazoonyeshwa kwenye chati. Bado wanaweza kupewa chanjo?

Ndiyo. Kuna ratiba maalum zinazoruhusu mtu yoyote aliyechelewa apokee chanjo zozote ambazo hakupata. Zungumza na daktari kuhusu njia bora zaidi ya kuhakikisha kwamba mtoto hakosi chanjo zake.

Mimi ni mtu mzima na sijapewa chanjo. Je, chanjo ni muhimu kwangu?

Ndiyo. Chanjo ni muhimu kwa kila mtu. Zinaweza kuwalinda watu wazima na watoto kutokana na magonjwa mengi hatari. Kupewa chanjo dhidi ya magonjwa yafuatayo: Matumbwitumbwi, Surua, Rubela, Polio, Pepopunda, Dondakoo, Patusisi, Homa ya Haemofilasi ya aina ya B, na Hepatiti B. Ikiwa unafikiria unahitaji chanjo, zungumza na daktari wako.

Chanjo zinaweza kufanya iwe vigumu kwa mwili kupambana na magonjwa?

Watu wengine wana wasiwasi kwamba chanjo hufanya iwe vigumu kwa mwili kutumia nyenzo zake kupambana na magonjwa. Kwa kweli, kinyume ndio kweli. Chanjo hufunza mwili kutumia uwezo wake asili kwa ufanisi ili kutambua magonjwa na kupambana nayo kabla ya wewe kuwa mgonjwa.

Chanjo zinaweza kumfanya mtoto wangu awe mgonjwa?

Chanjo haziwezi kukupa ugonjwa ambao zinafaa kukulinda dhidi yake. Pia hakuna ushahidi kwamba chanjo zinaweza kusababisha magonjwa mengine. Kuna uwezekano wa kuwa na mzio wa chanjo, lakini hali hizi huwa chache sana na ni kuna uwezekano mdogo ukilinganisha na magonjwa mabaya unayoweza kupata usipopewa chanjo.

Linda Familia Yako Kutokana na Magonjwa Hatari!

 • Dondakoo (DTaP/Tdap) – Ugonjwa mkali wa koo unaosababisha shida kupumua
 • Homa ya Haemofilasi ya aina ya B (Hib) – Ugonjwa unaoweza kuharibu masikio, macho, mapafu, na ubongo
 • Homa ya ini/Hepatiti A (HepA) – Ugonjwa wa ini ambao pia husababisha uchovu, kukosa tamaa ya chakula, na kichefuchefu
 • Homa ya ini/Hepatiti B (HepB) – Ugonjwa mkali wa ini, ambao wakati mwingine huwa wa muda mrefu unaosababisha saratani ya ini au ini kutofanya kazi
 • Virusi vya Papilamo kwa Watu (HPV) – Ugonjwa unaosababisha saratani ya uzazi kwa wanawake na saratani ya mkundu kwa wanawake na wanaume
 • Mafua – Ugonjwa wa msimu unaosababisha uchovu, homa, vidonda vya koo, na shida kupumua
 • Surua (MMR) – Ugonjwa mkali unaoenea haraka na unaweza kusababisha ukurutu na homa kali na kutosikia na kuharibu ubongo
 • Homa ya Uti wa Mgongo (MCV4) – Ugonjwa wa utando unaofunika ubongo na uti wa mgongo
 • Matumbwitumbwi (MMR) – Ugonjwa unaosababisha uvimbe wa mashavu na unaoweza kusababisha kutosikia na kuharibu ubongo, na utasa kwa wanaume
 • Patusisi (DTaP/Tdap) – Ugonjwa unaosababisha kikohozi kikali cha muda mrefu kinachosababisha ugumu wa kupumua
 • Ugonjwa wa Nimonia (PCV13) – Ugonjwa unaosababisha homa, ugumu wa kupumua, na unaweza kusababisha magonjwa mengine kadhaa
 • Polio (IPV) – Ugonjwa unaoweza kusababisha ulemavu wa kimwili wa maisha
 • Virusirota (RV) – Ugonjwa unaoweza kusababisha kutapika na kuharisha sana na hatimaye kusababisha kuishiwa na maji mwilini
 • Rubela (MMR) – Ugonjwa unaoweza kusababisha ukurutu katika mwili mzima na unaweza kuambukizwa mtoto wa mwanamke mjamzito
 • Pepopunda (DTap/Tdap) – Ugonjwa unaoweza kusababisha kukakaa kwa misuli na ugumu wa kupumua
 • Varisela (Var) – Ugonjwa unaoweza kusababisha ukurutu wa ngozi unaowasha na homa inayoweza kuwa hatari hasa kwa vijana, watu wazima, na wanawake wajawazito

Vyanzo

Idara ya Huduma za Afya ya Arizona Programu ya Kingamaradhi ya Arizona http://azdhs.gov/phs/ immunization/

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi