UMUHIMU WA MAVAZI

Maelezo ya jumla

Umuhimu wa mavazi -Tafiti nyingi zinaonesha kuwa, mavazi tunayovaa yana adhari kubwa kwa maisha yetu kiakili na kimwili. Japo tafiti hizi nyingi, ni tafiti ndogo, zinazofanyika kwa makundi ya watu wachache na hayajapata uwezekano wa kufanyika kwa watu wengi ulimwenguni, lakini kadri tafiti hizi zinavyoongezeka zinaashiria kuwa kuna kitu cha kibiolojia kinachotokea kwenye miili yetu tunapovaa mavazi mapya na kujihisi wapya pia.

Mavazi yanaweza kukufanya ujihisi mwenye kujiamini

“Nguvu ya tai” ni jambo halisi, kulingana na utafiti uliochapishwa katika jarida la Sayansi ya Saikolojia ya Kijamaa na Utu. Watafiti waliwachukua watu fulani watano na kuwavisha mavazi rasmi ya kibiashara na kuwapima uwezo wao katika kazi hiyo. Washiriki waliokuwa wamevaa mavazi rasmi walifanya kazi vyema zaidi na walionekana wenye nguvu na wanaojiamini zaidi kuliko washiriki wasiovaa mavazi rasmi.

Mavazi yanaweza kufanya uwezo wako wa kufikiria kuboreka

Mbali na kujihisi kuwa na nguvu zaidi, utafiti pia uligundua kuwa washiriki waliovaa mavazi rasmi walifikiri kwa haraka zaidi na walikuwa na maoni mengi ya kiubunifu. Wanasayansi walidokeza kuwa, jinsi unavyovyaa kunaweza kubadilisha mtazamo wako kuelekea vitu, watu, na hata matukio yanayokuzunguka – na kuchochea maoni, kupunguza usahaulifu na mtazamo mpya .umuhimu wa mavazi

Mavazi yanaweza kukufanya mtu makini

Kuvaa mavazi ambayo yanahusishwa na akili au umakini, kama vile kanzu ya daktari au sare za marubani, sio kwamba itakufanya uonekane nadhifu tu, bali pia yanaweza kukufanya uonekane mwenye akili zaidi, hii ni kulingana na tafiti iliyochapishwa katika Jarida la Saikolojia ya majaribio ya kijamii. Watafiti waliwapatia kanzu za daktari washiriki (ambao hawakuwa madaktari) na kisha kuwaagiza wafanye kazi kadhaa ngumu na tatanishi. Wale waliovaa vazi la daktari walifanya makosa machache sana kuliko watu waliovalia nguo zao za mtaani. Hata hivyo kati ya hao waliovaa kanzu za madaktari, nusu yao waliambiwa ni madaktari na nusu yao wakaambiwa ni wauza nyama. Tena, washiriki walioambiwa ni madaktari walifanya vyema zaidi kuliko walioambiwa ni wauza nyama buchani. Hii ilionesha kuwa sio tu unachovaa lakini pia ni muhimu unachofikiria kuhusu unachovaa.

Mavazi yanaweza kukutia motisha kufanya mazoezi

Unatamani kuanza kufanya mazoezi, lakini unakosa motisha? Jaribu kuvaa mavazi ya michezo. Watafiti wanasema kuvaa viatu vya michezo, kaptura na shati la michezo asubuhi kunaweza kukutia motisha unayohitaji kuanza mazoezi ili kupunguza hatari za magonjwa yatokanayo na uzito mkubwa au kitambi.

Nguo unazovaa zinaweza kukufanya upunguze uzito

Kuvaa nguo au mkanda unaoshika kiuno au tumbo, kutasaidia kutambua pindi tu unapohisi kushiba ili uache kula. Baadhi ya wanawake hufunga mshipi tumboni ili kuwataarifu wapofikia kushiba ili waache kula inapoanza kukaza, hasa wanapokuwa katika hafla.

Mavazi yanaweza kukufanya uwe na furaha

Mara nyingi tunavaa mavazi sawa na tunavyojihisi au tunavyotaka kuhisi au jinsi tunavyotaka wengine wadhani tunajihisi. Na mara nyingi hili linafanya kazi , hasa kama tumewahi kusifiwa baada ya kuvaa aina fulani ya mavazi au kama yanaleta kumbukumbu njema ya matukio ya zamani. Unapojihisi kushuka moyo, kuvaa vizuri na kujumuika na marafiki kunaweza kufukuzia mbali msongo na sonona

Angalizo

Mavazi unayovaa yanaweza kubadili jinsi watu wanavyokusiliza na jinsi wanavyoelewa unachosema, kuvaa vizuri hubadili jinsi wewe na watu wengine wanavyokuona.  Uvaaji wako unaweza kupunguza au kuongeza  umuhimu wa kile unachosema,hasa kwa watu wanaokusikiliza na wanaokutazama.
Haijalishi unataka kutuma ujumbe gani kwa dunia, kumbuka kuwa mavazi unayoweka ujumbe huo, yanaweza kuamua jinsi utakavyopokelewa. Kuwa makini unapovaa….

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/patientinstructions/000817.htm

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi