UPUNGUFU WA MAJI MWILINI

UPUNGUFU WA MAJI MWILINI

 • January 19, 2021
 • 0 Likes
 • 111 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Upungufu wa maji mwilini (Dehydration) unaweza kuwa upungufu wa kadri, upungufu wa wastani, au upungufu mkubwa sana kulingana na kiasi cha maji ya mwili yaliyopotea. Upungufu wa maji mwilini unapokuwa mkubwa sana unaweza kutishia maisha.

Upungufu wa maji mwilini humaanisha kuwa mwili wako hauna maji ya kutosha inavyopaswa.

Dalili za upungufu wa maji mwilini?

 • Midomo mikavu
 • Uchovu au koma (kama kuna upungufu mkubwa sana wa maji mwilini)
 • Kiasi cha mkojo hupungua sana, mkojo huwa wa njano sana
 • Hakuna machozi
 • Macho hudumbukia ndani
 • Utosi wa mtoto mchanga hudumbukia ndani

Ni nini husababisha upungufu wa maji mwilini?

Upungufu wa maji mwilini husababishwa na kupotea kwa maji mengi kutoka mwilini au kutokunywa maji ya kutosha.

Mwili wako unaweza kupoteza maji mengi kwa:

Unaweza usinywe maji ya kutosha kama:

Upungufu wa maji mwilini kwa watoto husababishwa na kukataa kula au kunywa na kupoteza maji mwilini kwa kutapika, kuharisha na homa. Watoto wadogo na watoto wachanga wako kwenye hatari zaidi ya kuishiwa maji mwilini kuliko ilivyo kwa watu wazima. Hii ni kwa sababu ya uzito wao mdogo na miili yao kupoteza maji haraka sana kuliko ilivyo kwa watu wazima. wazee na watu wazima wanaougua wako kwenye hatari zaidi pia.

Utambuzi

Dakitari anaweza kufanya uchunguzi wa mwili na kuona ishara zifuatazo:

 • Kushuka kwa shinikizo la damu mgonjwa aliyelala anapokaa au kusimama.
 • Kushuka kwa shinikizo la damu.
 • Kusinyaa kwa ngozi ya mwili- Unapofinya ngozi ya mtu mwenye upungufu wa maji, haijivuti kama ilivyo kawaida na inachukua muda kurudi katika hali yake ya mwanzo.
 • Kuongezeka kwa mapigo ya moyo
 • Mshtuko-shock

Vipimo vinavyoweza kufanyika ni pamoja na:

 • Vipimo vya damu kuangalia kiwango cha madini, kama vile sodiamu, potasiamu, na bicarbonates yaliyobakia mwilini -electrolytes
 • Kipimo cha damu kinachofanyika kuangalia kwango cha urea kwenye damu-BUN
 • Kipimo cha kuhesabu kiwango cha seli zilizo kwenye damu-CBC
 • Creatinine
 • Kuangalia uzito wa mkojo –specific gravity

Vipimo vingine vinaweza kufanywa ili kujua sababu ya upungufu wa maji mwilini (kwa mfano, kiwango cha sukari kwenye damu ili kuangalia ugonjwa wa sukari).

Wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Mwone daktari kama wewe au mwanao ana dalili zifuatazo:

Fika kituo cha afya kama wewe au mwanao ana dalili zifuatazo:

 • Kama kuna damu kwenye kinyesi au matapishi
 • Kuhara au kutapika (kwa watoto wachanga chini ya miezi 2)
 • Midomo mikavu au macho makavu
 • Ngozi kavu na iliyosinyaa, inarudi polepole mahala pake baada ya kufinywa.
 • Moyo unaodunda haraka
 • Kupata mkojo kidogo au kutopata kabisa kwa masaa manane au zaidi.
 • Kma hauna machozi
 • Kma una macho yaliyodumbukia ndani
 • Kama utosi wa mtoto mchanga umedumbukia ndani

Ongea na mtumishi wa afya kama unadhani kiasi cha maji unachompatia mwanao hakimtoshi.

Pia, ongea na mtumishi wa afya kama:

 • Kama wewe au mwanao mgonjwa anashindwa kula chochote au kunywa chochote bila kutapika au kuharisha.
 • Kama umekuwa ukitapika kwa zaidi ya masaa 24 kwa mtu mzima au kwa zaidi ya masaa 12 kwa mtoto
 • Kama kuhara kumedumu kwa zaidi ya siku 5 kwa mtu mzima au mtoto
 • Kma mwanao mchanga au mwanao mkubwa amenyong’onyea sana kuliko kawaida
 • Kma wewe au mwanao anakojoa sana kuliko kawaida, hasa kama kuna historia ya kisukari kwenye familia yako au kama unatumia madawa ya kupunguza maji mwilini

Uchaguzi wa matibabu

Kunywa maji ya kutosha husaidia kuondoa upungufu wa kadiri wa maji mwilini. Ni vizuri zaidi kunywa maji kidogo kidogo (kwa kutumia kijiko au bomba la sindano kwa watoto wachanga), badala ya kujilazimisha kunywa maji mengi sana kwa wakati mmoja. Kunywa maji mengi sana kwa wakati mmoja kunaweza kusababisha utapike zaidi.

Tumia mchanganyiko wa ORS-Oral Rehydration Salt ili kutibu upungufu wa maji kama mtoto anaweza kunywa. Ongea na daktari wako atakuelekeza jinsi ya kuichanganya na jinsi ya kuitumia. Usitumie maji ya kawaida kumtibu mtu anayehara sana. Maji ya kawaida hayana madini na chumvichumvi za kutosha kuurejesha mwili katika hali yake.

Wagonjwa wenye upungufu wa maji wa wastani au mkubwa sana wanaweza kulazwa hospitalini ili kuongezewa maji kwenye mishipa yao. Tiba ya aina hii huwafaa zaidi wagonjwa waliopoteza fahamu au walionyong’onyea sana. Baadae wakiweza kula na kunywa tena huanza kupewa ORS.

Mtoa huduma za afya atajaribu kutambua sababu ya kuhara au kutapika kwako na kuishughulikia.

Kesi nyingi za kuharisha na kutapika husababishwa na virusi, kwa hiyo zinapona zenyewe bila matibabu yoyote.

Madawa ya kuepuka

Wagonjwa waliotambuliwa kuwa wana upungufu wa maji mwilini, wanapaswa kuepuka kutumia dawa zifuatazo:

 • Iopromide
 • Mannitol
 • Methenamine

Kama umetambuliwa kuwa una upungufu wa maji mwilini, ongea na daktari kabla ya kuanza au kuacha dawa yoyote

Kuzuia

Hata unapokuwa na afya njema, kunywa maji mengi kila siku. Kunywa mengi zaidi kunapokuwepo na joto au wakati unapofanya mazoezi.

Kuwa mwangalifu unapowahudumia wagonjwa, hasa watoto wachanga, watoto wakubwa au wazee. Kama ukihisi kuwa mgonjwa anapata upungufu wa maji , mwone mtoa huduma za afya kabla hali haijawa mbaya zaidi. Mpatie maji mgonjwa baada tu ya kuanza kuharisha au kutapika. USISUBIRI mpaka utakapoona dalili za upungufu wa mwili.

Mara zote, mshauri mtu yeyote anayeumwa anywe maji ya kutosha. Kumbuka pia mahitaji ya maji mwilini huongezeka wakati wa homa mwilini, kutapika au kuharisha. Njia rahisi ya kuwaangalia wagonjwa ni kuangalia kiasi cha mkojo anachotoa.

Nini cha kutarajia?

Kama upungufu wa maji utatambuliwa mapema na kutibiwa , matokeo yatakuwa mazuri.

Mtatizo yanayoweza kutokea

Kma upungufu mkubwa sana wa maji hautarekebishwa inaweza kusababisha:

 • Kifo
 • Uharibifu wa kudumu wa ubongo
 • Mshtuko

Vyanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/000982.htm

 

 • Share:

Leave Your Comment