Magonjwa ya ndani ya mwili

USAFI WA MKONO

Usafi wa mikono

Maelezo ya jumla

Tanzania inapatikana katika eneo la kitropiki, kuna vimelea wengi kwenye:

  • Vumbi
  • Udongo
  • Karibu kila kitu tunachogusa

Lakini pia, kwa sababu ya mazingira ya joto tunayoishi, hali ya hewa inasababisha kutokwa jasho na mafuta kwenye mikono yanayoruhusu kukua na kuongezeka kwa vimelea. Kushindwa kusafisha vyema mikono ni njia moja wapo ya kusababisha magonjwa kusambaa. Kama kucha za mikono hazijakatwa vizuri, zinaweza kutunza uchafu mwingi.

Matatizo yanayotokana na kucha chafuusafi wa mikono

Kama kucha hazitakuwa safi zinaweza kusababisha matatizo yafuatayo:

  • Kupata magonjwa ya ngozi baada ya kujikwaruza na kusambaza vimelea kwenye ngoi
  • Minyoo inaweza kujificha kwenye kucha na baadae kuingizwa mdomoni wakati wa kula
  • Kuchafua chakula wakati wa kukiandaa. Uwezekano wa kupata magonjwa kwa njia hii ni mkubwa kama mikono inaandaa chakula mara kwa mara.

Kunawa mikono kila baada ya kutoka chooni au kabla ya kuandaa chakula ni sehemu muhimu ya usafi binafsi

Vifaa vya kunawia mikono

Kwa kaya nyingi zinazoishi katika miji ya Tanzania, miundombinu ya kunawa mikono haiko sawa kwa sababu za kiuchumi na kukosa maji ya bomba. Lakini kukosekana kwa miundombinu hii haikuzuii kunawa mikono.

Vifaa va kunawia mikono vinaweza kutengenezwa kwa kutumia vifaa vilivyo ndani ya nyumba. Kwa upande mwingine, kama kutengeneza hakuwezekani, unaweza kutumia beseni na jagi kumwagia maji.

Kwa ubora zaidi unaweza kutengeneza sehemu ya kunawia mikono kwa kutumia chungu kilichotengeneza kwa matope au plastic. Unaweza kutoboa tundu chini ya chombo na kuweka kizibo kitakachozuia maji kuvuja.

Chungu cha kunawia kinaweza kutengenezwa moja kwa moja na mfinyanzi au unaweza kutumia kisu kutoboa taratibu chungu kilichopo tayari kwa matumizi na kisha kukiwekea kizibo.

Vifaa kama hivi vinapaswa kuning’inizwa kwa nje ili iwe rahisi kwa wanafamilia kunawa mikono wanapotoka chooni, kabla ya kula au baada ya kushika uchafu.

Mambo ya kufanya kupunguza usambazaji wa magonjwa kwa mikonoUsafi wa mikono

  • Hakikisha kucha zako ni safi kila wakati
  • Hakikisha kucha zimekatwa vizuri na ziwe fupi
  • Tumia sabuni kunawa kabla na baada ya kula
  • Tumia sabuni kunawa kila baada ya kutoka chooni
  • Tumia sabuni kunawa kabla ya haujaanza kuandaa chakula

Kutokunawa mikono vizuri ni sawa na kutokunawa kabisa. Imekuwa kawaida kwa watu, hata wasomi, kunawa mikono haraka na bila kutumia sabuni. Hautapunguza vimelea wa kutosha kutoka kwenye mikono kama utanawa haraka na bila sabuni.

Tunahitaji kujielimisha wenyewe na kisha tuwaelimishe wengine kuhusu hili. Kama hauna sabuni ya kutumia, jaribu kunawa mikono kwa muda mrefu zaidi (kama sekunde 30), au baada ya kutoka chooni au baada ya kushika uchafu, mtu anaweza kunawa mikono kwa majivu. Kunawa mikono kwa kutumia majivu kunaongeza msuguano na kuondoa vimelea wengi zaidi.

Jifunze zaidi hapa kuhusu kusafisha;

Vyanzo

https://www.betterhealth.vic.gov.au/health/conditionsandtreatments/personal-hygiene

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X