UTANGOTANGO/MATANGATANGA/MBA WA MWILI

Maelezo ya jumla

Utangotango/matangatanga/mba wa mwili (tinea versicolor) ni maambukizi ya fangasi kwenye ngozi yanayodumu kwa muda mrefu.

Ni zipi dalili za utangotango/matangatanga/mba wa mwili?utangotango

Dalili kuu ni kuwepo kwa mabaka kwenye ngozi yenye rangi iliyofifia, yana kingo zilizonyooka na zinaonekana kama magamaba mepesi. Mabaka kwa kawaida yana rangi ya wekundu iliyofifia. Maeneo yanayotokewa zaidi na utangotango/matangatanga/mba wa mwili ni mgongoni, kwenye makwapa, mikono, kifua, na shingo. Sehemu iliyoathirika rangi yake inaonekana kufifia kuliko sehemu nyingine.

Kwa watu weusi, unaona kama ngozi inapoteza rangi au unaona rangi ya eneo lililoathirika linafifia.

Dalili nyingine ni pamoja na:

Ni nini husababisha utangotango/matangatanga/mba wa mwili?

Utangotango/matangatanga/mba wa mwili unawapata watu wengi. Unasababishwa na fangasi aanayeitwa “pityrosporum ovale”, huyu ni aina ya fangasi ambaye hupatikana kwenye ngozi ya mwanadamu. Aina hii ya fangasi husababisha matatizo katika hali fulani maalumu tu.

Nani yuko kwenye hatari zaidi ya kupata utangotango/matangatanga/mba wa mwili?

Tatizo la utangotango/matangatanga/mba wa mwili linawapata zaidi vijana wanaobalehe na vijana wanaume. Mara nyingi utangotango unatokea wakati wa joto.

Utambuzi wa utangotango/matangatanga/mba wa mwili

Daktari atakwangua ngozi ya sehemu yenye utangotango/matangatanga/mba wa mwili kuchukua sampuli, na kisha kuichunguza chini ya darubini kuona fangasi.

Ni wakati gani upaswa kuomba msaada wa kitabibu?matangatanga

Ongea na daktari kama unaona una dalili yoyote ya utangotango/matangatanga/mba wa mwili.

Uchaguzi wa matibabu

Matibabu yanahusisha kuweka dawa ya kudhibiti fangasi kwenye ngozi. Dawa hizi ni kama vile clotrimazole, ketoconazole, na miconazole.

Unaweza pia kutumia shampoo zinazopatikana duka la dawa (dandruff shampoo) na kuzipaka kwenye ngozi kwa dakika 10 kila siku unapooga itasaidia.

Matarajio

Japo ugonjwa wa utangotango/matangatanga/mba wa mwili unatibika kiurahisi, mabadiliko ya rangi ya ngozi yanaweza kubakia kwa miezi kadhaa bada ya matibabu. Shida ya utangotango/matangatanga/mba wa mwili inaweza kujirudia wakati wa joto.

Kuzuia

Watu wenye historia ya kupata utangotango/matangatanga/mba wa mwili wanapswa kuepuka kutokwa jasho sana au joto kali

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001465.htm

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi