UTUNZAJI SALAMA WA CHAKULA

Nunua vyakula vilivyo salamachagua chakula

 1. Ili kuwa na chakula salama, usinunue mayai yaliyo na nyufa hata kama yanauzwa kwa bei nafuu.
 2. Usinunue matunda na mboga za majani zilizochubuka au zenye madoa ya kuoza.
 3. Usile mayai mabichi au chakula kilichochanganywa na mayai mabichi.
 4. Usile vyakula vilivyoshambuliwa na fangasi.
 5. Kagua tarehe ya kumalizika muda wa matumizi ya vyakula vilivyotengenezwa viwandani na usinunue au kutumia vyakula vilivyopita muda wa kutumika.
 6. Usinunue vyakula vilivyopakiwa kwenye kontena/chombo ambacho mfuniko umepasuka au kwenye makopo yaliyobondeka.
 7. Epuka kula vyakula vya mitaani kwa sababu huenda vikawa havikuandaliwa katika hali ya usafi

Andaa chakula kwa usafi

 1. Safisha vyombo vya kuandalia na kupakulia chakula kwa sabuni na suuza kwa maji safi yanayotiririka.
 2. Nawa mikono kabla ya kuandaa chakula. Funika vidonda na michubuko katika mikono yako kabla ya kushika au kuandaa chakula.
 3. Tumia maji safi yaliyochemshwa au kutibiwa kwa kusafishia matunda au mboga mboga zinazoliwa mbichi. Tumia mbao au sehemu tofauti za kukatia nyama mbichi/samaki wabichi na kwa kukatia matunda au mbogamboga.
 4. Pika vyakula vibichi kwa muda mrefu mfano nyama, kuku, mayai, samaki na vyakula vingine vya baharini. Kwa nyama na kuku, hakikisha supu ina rangi nyeupe na siyo ya pinki. Acha mchuzi na supu vichemke vizuri.
 5. Pasha moto viporo mpaka viwe na moto ambao huwezi kugusa. Koroga wakati unapasha moto.

Hifadhi chakula kwa usafi

 1. Usiache vyakula vilivyopikwa nje kwa muda wa zaidi ya saa 2. Usihifadhi mayai mabichi kwa zaidi ya wiki 4; mayai yaliyochemshwa, maziwa freshi au mtindi isiwe zaidi ya wiki 1; nyama au samaki isiwe zaidi ya siku 2; au vyakula vilivyopikwa isiwe zaidi ya siku 4.
 2. Andaa vyakula freshi kwa ajili ya watoto wachanga, watoto wadogo, vijana au watu wenye maambukizi ya VVU na hifadhi baada ya kuvipika.
 3. Kinga vyakula visishambuliwe na wadudu wa majumbani kwa kuvifunika au kuvihifadhi katika kontena iliyofunikwa.

Vyanzo

https://www.tfnc.go.tz/publications/9

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi