Lishe

UWIANO WA UZITO NA UREFU (BMI):Njia ya kutathmini uzito wa mwili

BMI

Last Updated on October 12, 2023 by Dr Mniko

Uwiano wa uzito na urefu

Uwiano wa uzito na urefu – Uwiano wa uzito katika kilogramu na urefu katika mita hupatikana kwa kutumia kanuni ifuatayo:

BMI = Uzito (Kg)/ Urefu (m) x Urefu (m)

Uwiano wa uzito na urefu
BMI

BMI huwa na viwango mbalimbali vilivyowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kutafsiri hali ya lishe ya mtu, ambavyo ni:

  • BMI chini ya 18.5 = Uzito Pungufu
  • BMI kati ya 18.5 mpaka 24.9 = Uzito unaofaa
  • BMI kati ya 25.0 na 29.9 = Unene uliozidi
  • BMI ya 30.0 au zaidi = Unene uliokithiri au kiribatumbo

Mahitaji ya chakula mwilini hutegemea umri, jinsia, hali ya kifiziolojia (kama ujauzito au kunyonyesha), hali ya kiafya, kazi na mtindo wa maisha. Uzito wa mwili hutegemea kiasi na aina ya chakula unachokula; pamoja na shughuli unazofanya. Mara nyingi unene hutokana na kula chakula kwa wingi kuliko mahitaji ya mwili na kutofanya mazoezi. Endapo kiasi cha chakula unachokula kinatoa nishati-lishe nyingi kuliko mahitaji ya mwili, ziada hii huhifadhiwa mwilini kama mafuta hivyo kuongezeka kwa uzito wa mwili. Unene uliokithiri unachangia kwa kiwango kikubwa kupata magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza kama kisukari, magonjwa ya moyo, shinikizo kubwa la damu na saratani. Endapo BMI ni kubwa ushauri kuhusu ulaji unaofaa na mtindo wa maisha utolewe na mbinu za kupunguza uzito zijadiliwe.

Epuka kuwa na uzito mkubwa kwa:

  • Kutumia mafuta kwa kiasi kidogo;
    • Kuepuka vyakula vyenye mafuta mengi hususan vinavyopikwa kwa kudumbukizwa kwenye mafuta au kukaangwa kwa mafuta mengi;
  • Kuepuka matumizi ya vinywaji au vyakula vyenye sukari nyingi;
    • Kuepuka asusa zenye mafuta mengi au sukari nyingi kati ya milo; na
  • Kuongeza vyakula vyenye makapi-mlo kwa wingi kama matunda, mbogamboga na nafaka zisizokobolewa.

Kumbuka: ­

  • BMI haitumiki kwa wanawake wajawazito ­
  • BMI inapotumika kwa watoto na vijana walio katika umri chini ya miaka 18, chati maalumu ambayo inahusisha umri na jinsia hutumika kuonyesha hali ya lishe ya wahusika. Hivyo ni rahisi zaidi kutumika kwa watu wazima. ­
  • BMI haitumiki kwa walengwa wasioweza kusimama vyema, waliovimba miguu na wanawake wanaonyonyesha katika miezi 6 ya mwanzo baada ya kujifungua.

Vyanzo

https://www.tfnc.go.tz/publications/9

Leave feedback about this

  • Quality
  • Price
  • Service

PROS

+
Add Field

CONS

+
Add Field
Choose Image
Choose Video
X