VIDONGE VYA DHARURA VYA KUZUIA MIMBA

Vidonge vya Dharura vya Kuzuia Mimba ni nini?

Vidonge vya dharura vya kuzuia mimba ni vidonge ambavyo vina projestini pekee, au projestini na estrojeni kwa pamoja – vichocheo vilivyo kama vichocheo asilia vya projestini na estrojeni kwenye mwili wa binadamu.

 • Vidonge vya dharura kuzuia mimba wakati mwingine huitwa vidonge vya “morning after” au “postcoital contraceptives.
 • Hufanya kazi kimsingi kwa kuzuia au kuchelewesha kuachiwa kwa yai kutoka kwenye ovari (uovuleshaji). Hazifanyi kazi kama mwanamke tayari ni mjamzito

Mambo Muhimu kuhusu vidonge vya dharura vya kuzuia mimba

 • Vidonge vya dharura kuzuia mimba husaidia kuzuia mimba kama vitamezwa katika muda usiozidi siku 5 baada ya ngono bila kinga. Vikimezwa mapema zaidi, ni bora.
 • Havikatishi mimba iliyoshika.
 • Salama kwa wanawake wote – hata wanawake ambao hawawezi kutumia njia zilizopo za vichocheo kwa ajili ya kuzuia mimba.
 • Hutoa fursa kwa wanawake kuanza kutumia njia zilizopo za uzazi wa mpango.
 • Njia nyingi zinaweza kutumika kama vidonge vya dharura kuzuia mimba. Bidhaa bora, vidonge vyenye projestini, na vidonge vyenye vichocheo viwili vyote vinaweza kutumika kama njia za dharura za kuzuia mimba.

Ni Vidonge Gani Vinaweza Kutumika kama Vidonge vya Dharura Kuzuia Mimba?

 • Kuna bidhaa kadhaa zinazoweza kutumika
  • Bidhaa maalum ya Vidonge vya Dharura Kuzuia Mimba vyenye progestin levonorgestrel
  • Bidhaa maalum ya Vidonge vya Dharura Kuzuia Mimba vyenye estrojeni na levonorgestrel
  • Vidonge vyenye projestini na levonorgetrel au norgestrel
  • Vidonge vyenye vichocheo viwili vyenye ostrojeni na projestini – levovorgestrel, norgestrel, au norethindrone (inayoitwa pia norethisterone)
 • Mtaalamu wa afya atakupatia moja ya hizi

Vidonge Vya Dharura Vya Kuzuia Mimba Vimezwe Wakati Gani?

 • Mapema iwezekanavyo baada ya kufanya ngono bila kinga (ngono isiyo salama). Vidonge vya dharura kuzuia mimba vikimezwa mapema baada ya ngono isiyo salama, ndivyo vinavyoweza kuzuia mimba vizuri zaidi.
 • Vinaweza kuzuia mimba kama vitamezwa ndani ya siku zisizozidi tano (5) baada ya ngono isiyo salama.

Vidonge vya Dharura Vya Kuzuia Mimba Vina Ufanisi Kiasi Gani?

 • Kama wanawake 100 kila mmoja amefanya ngono mara moja katika wiki ya pili au ya tatu ya mzunguko wa hedhi bila kutumia kinga, wanawake wanane (8) wana uwezekano wa kupata mimba.
 • Kama wanawake 100 wametumia Vidonge vya Dharura Kuzuia Mimba vyenye projestini tu, mmoja (1) ana uwezekano wa kupata mimba.
 • Kama wanawake 100 walitumia Vidonge vya Dharura Kuzuia Mimba vyenye estrojeni na projestini, wawili (2) wanawezekana kupata mimba.

Kuhusu Athari za Dawa

Madhara yanayofahamika zaidi Kupata hedhi ya damu kidogo isivyo kawaida kwa siku 1-2 baada ya kumeza Vidonge vya Dharura Kuzuia Mimba.
Hedhi ambayo huanza mapema au kuchelewa kuliko ilivyotarajiwa
Maumivu ya kichwa, maumivu ya matiti, kizunguzungu, kichefuchefu, maumivu ya tumbo, uchovu, kutapika
Ufafanuzi kuhusu madhara haya Yanaweza kuwa yamesababishwa au hayakusababishwa na njia anayotumia
Hedhi isiyotabirika kutokana na Vidonge Vya Dharura Kuzuia Mimba itakoma bila tiba. Hii si dalili ya ugonjwa au ujauzito.
Hedhi inaweza kuanza mapema au baadaye kuliko ilivyotarajiwa. Hii si dalili ya ugonjwa au ujauzito.
Kama hedhi yako ya mwezi unaofuata itaendelea kwa zaidi ya wiki moja kuliko ilivyotarajiwa baada ya kumeza Vidonge vya Dharura Kuzuia Mimba, fanya uchunguzi wa ujauzito.
Hakuna hatari zinazojulikana kwa kijusi kilichotungwa kama Vidonge vya Dharura Kuzuia Mimba vitashindwa kuzuia kupata mimba

 

Faida na Hasara za kutumia vidonge

Faida za Kiafya Hasara  Kiafya
Husaidia kukinga dhidi ya hatari ya kupata mimba Hakuna

 

Nani Anaweza Kutumia Vidonge vya Dharura Kuzuia Mimba

 • Ni Salama na Vinafaa kwa Wanawake Wote
 • Si lazima kupima na kufanya uchunguzi ili kutumia Vidonge vya Dharura Kuzuia Mimba. Vinaweza kuwa sahihi kwa sababu nyingine – hasa kama ngono ilikuwa ya kutumia mabavu
 • Wanawake wote wanaweza kutumia Vidonge vya Dharura Kuzuia Mimba kwa usalama na ipasavyo, pamoja na wanawake ambao hawawezi kutumia njia zilizopo zenye vichocheo kuzuia mimba. Kwa sababu ya kutumiwa kwa muda mfupi, hakuna masharti ya tiba ambayo yanafanya Vidonge vya Dharura Kuzuia Mimba kuwa hatari kwa mwanamke.

Vidonge vya Dharura Vitumiwe Wakati Gani

Wakati wowote ndani ya siku 5 baada ya ngono bila kinga. Vidonge vya Dharura Kuzuia Mimba vikimezwa mapema zaidi baada ya ngono bila kinga, ndivyo vinavyoweza kufanya kazi vizuri zaidi.

Vidonge vya Dharura Kuzuia Mimba vinaweza kutumika wakati wowote mwanamke anapopata wasiwasi kuwa anaweza kupata mimba. Kwa mfano, baada ya:

 • Ngono ya kulazimishwa (kubakwa) au kushurutishwa
 • Ngono yoyote bila kinga
 • Makosa ya kutumia njia ya uzazi wa mpango, kama vile:
  • Kondomu haikutumika kwa usahihi, ilichomoka, au kupasuka
  • Wenza walitumia kwa makosa njia ya kalenda (kwa mfano, walishindwa kujizuia kufanya ngono au kutumia njia nyingine ya kuzuia mimba katika siku zenye hatari ya kushika mimba)
  • Mwanaume ameshindwa kushusha kando, kama ilivyokusudiwa, kabla ya kumwaga manii
  • Mwanamke amepitisha muda bila kumeza vidonge 3 au zaidi vya uzazi wa mpango au amechelewa kuanza paketi mpya siku tatu au zaidi
  • Kitanzi kimechomoka
  • Mwanamke amechelewa zaidi ya wiki mbili kuchoma sindano ya projestini au amechelewa zaidi ya siku 7 kuchoma sindano yake ya mwezi

Namna ya kutumia Vidonge vya dharura Kuzuia mimba

 • Mtaalamu atakupatia aina moja ya vidonge vya dharura
  • Unaweza kuelekezwa kumeza vidonge mara moja tu au
  • Unaweza kupewa vidonge vyevye kipimo cha dozi mbili, na utapaswa kumeza dozi nyingine baada ya masaa 12
 • Nini cha kufanya kuhusiana na madhara
  • Kichefuchefu:
   • Haishauriwi kuzoea kumeza dawa za kuzuia kichefuchefu
   • Wanawake ambao walishapata kichefuchefu walipomeza Vidonge vya Dharura Kuzuia Mimba safari iliyopita au walipomeza dozi ya kwanza ya kipimo cha dozi 2 wanaweza kutumia dawa za kuzuia kati ya nusu saa hadi saa moja kabla ya kumeza Vidonge vya Dharura Kuzuia Mimba
  • Kutapika:
   • Kama mwanamke atatapika ndani ya saa 2 baada ya kumeza Vidonge vya Dharura Kuzuia Mimba, lazima ameze dozi nyingine. (Anaweza kutumia dawa za kuzuia kichefuchefu anaporudia kumeza dozi).
   • Kama kutapika kutaendelea, anaweza kurudia dozi kwa kuingiza vidonge kwenye uke wake.
   • Kama itatokea kutapika ndani ya saa 2 baada ya kutumia Vidonge vya Dharura Kuzuia Mimba, hana haja ya kumeza vidonge tena

Imani potofu zilizopo kwenye jamii

Vidonge vya Dharura Kuzuia Mimba:

 • Havisababishi mimba kutoka.
 • Havisababishi mtoto kuzaliwa na kasoro kama itatokea kupata mimba.
 • Si hatari kwa afya ya mwanamke.
 • Havikuzi tabia ya kutojali hatari ya ngono.
 • Haviwafanyi wanawake kuwa wagumba.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/birthcontrol.html

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi