Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko
Vidonge vyenye kichocheo kimoja vya kupanga uzazi ni Nini?
Vidonge vyenye kichocheo kimoja vya kupanga uzazi ni vidonge ambavyo vina dozi ndogo sana ya projestini kama kilivyo kichocheo cha asili cha projesteroni kwenye mwili wa mwanamke.
- Havina estrojeni, na hivyo vinaweza kutumiwa wakati wote wa kunyonyesha maziwa ya mama na wanawake ambao hawawezi kutumia vidonge vyenye estrojeni.
- Vidonge vyenye kichocheo kimoja pia vinajulikana kama “minipills” na vidonge vyenye vichocheo viwili vyenye projestini tu.
- Hufanya kazi hasa kwa:
- kutengeneza utando mzito kwenye shingo ya mji wa mimba (huu huzuia mbegu za kiume zisikutane na yai)
- huvuruga mzunguko wa hedhi, pamoja na kuzuia mayai ya mwanamke yasipevuke kwenye ovari (uovuleshaji).
Mambo Muhimu kuhusu vidonge vyenye kichocheo kimoja
- Meza kidonge kimoja kila siku. Usiache kumeza kidonge wakati wa kubadili paketi moja hadi nyingine.
- Salama kwa wanawake wanaonyonyesha maziwa ya mama na watoto wao. Vidonge vyenye kichocheo kimoja haviathiri uzalishaji wa maziwa.
- Husaidia kuongezea uwezo wa kuzuia mimba kutokana na kunyonyesha maziwa ya mama. Kwa pamoja, hutoa kinga madhubuti ya kuzuia mimba.
- Mabadiliko ya hedhi ni ya kawaida lakini hayana madhara. Kwa kawaida vidonge huongeza muda wa wanawake wanaonyonyesha kutopata hedhi. Kwa wanawake kupata hedhi mara kwa mara au zisizotabirika ni jambo la kawaida.
- Zinaweza kutolewa kwa mwanamke wakati wowote aanze kuzimeza baadaye. Kama haiwezekani kugundua ujauzito, mtoa huduma anaweza kumpatia vidonge ameze baadaye, atakapoanza kupata hedhi
Vidonge vyenye kichoina Ufanisi Kiasi Gani?
Ufanisi unategemeana na mtumiaji. Kwa wanawake ambao wanapata hedhi, hatari ya kupata mimba ni kubwa sana kama vidonge vitachelewa kumezwa au kuacha kumezwa kabisa.
Wanawake wanaonyonyesha:
- Kama ilivyozoeleka, hutokea karibu mimba 1 kwa wanawake 100 wanaotumia Vidonge vyenye kichocheo kimoja kwa mwaka wa kwanza. Hii ina maana kuwa wanawake 99 kati ya 100 hawatapata mimba.
- Vidonge vikimezwa kila siku, kutakuwa na chini ya mimba 1 kwa wanawake 100 wanaotumia vidonge vyenye kichocheo kimoja kwa mwaka wa kwanza (wanawake 3 kwa 1,000).
Vina mafanikio kidogo kwa wanawake wasionyonyesha:
- Kama kawaida, kunakuwa na karibu mimba 3 hadi 10 kwa wanawake 100 wanaotumia vidonge vyenye kichocheo kimoja kwa mwaka wa kwanza. Hii ina maana kuwa wanawake 90 hadi 97 kati ya kila 100 hawatapata mimba.
- Vidonge vikimezwa kila siku kwa wakati uleule, kutakuwa na chini ya mimba moja kwa wanawake 100 wanaotumia vidonge vyenye kichocheo kimoja kwa mwaka wa kwanza (wanawake 9 kati ya 1,000).
Kuhusu Athari za Dawa
- Madhara yanayofahamika zaidi
- Wanawake wanaonyonyesha watoto kwa kawaida hawapati hedhi kwa miezi kadhaa baada ya kuzaa, vidonge vyenye projestini hurefusha kipindi hiki.
- Wanawake ambao hawanyonyeshi wanaweza kuwa na hedhi mara kwa mara au isiyotabirika kwa miezi kadhaa ya kwanza, ikifuatiwa na hedhi ya kawaida au kuendelea hedhi isiyotabirika.
- Maumivu ya kichwa, kizunguzungu, maumivu ya matiti, Mabadiliko ya hisia, maumivu ya tumbo na madhara mengine yanayoweza kutokea.
- Ufafanuzi kuhusu madhara haya
- Madhara si dalili za ugonjwa.
- Kwa kawaida hupungua au kuacha ndani ya miezi michache ya kwanza ya kumeza vidonge vyenye projestini. Hedhi hubadilika, hata hivyo, kawaida huendelea.
- Madhara ni ya kawaida lakini baadhi ya wanawake hayawapati
- Fanya yafuatayo ukipata madhara haya
- Endelea kumeza vidonge vyenye projestini. Kuacha kumeza vidonge huleta hatari ya mimba.
- Jaribu kumeza vidonge wakati wa kula au wakati wa kulala ili kusaidia kukumbuka.
- Mteja anaweza kurudi kwa ajili ya kupata msaada kama madhara yanamsumbua.
Faida na Hasara za kutumia vidonge
Faida za Kiafya | Hasara Kiafya |
Husaidia kukinga dhidi ya mimba | Hakuna |
Nani Anaweza kutumia Vidonge vyenye kichocheo kimoja
Karibu wanawake wote wanaweza kutumia vidonge vyenye kichocheo kimoja kwa usalama, ikiwa ni pamoja na wanawake ambao:
- Wanaonyonyesha (wanaweza kuanza mapema wiki sita baada ya kujifungua)
- Wameshazaa na ambao bado hawajazaa watoto
- Hawajaolewa
- Wa umri wowote, pamoja na vijana na wanawake wenye umri zaidi ya miaka 40
- Wametoa tu mimba, mimba imeharibika, au wamepata mimba iliyotunga nje ya kizazi
- Wanavuta sigara, bila kujali umri wa mwanamke au idadi ya sigara anazovuta
- Wana anemia sasa waliipata siku za nyuma Wana vena zilizojikunja
- Wameambukizwa VVU, hata kama wanatumia au hawatumii dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (antiretroviral)
Nani hawezi kutumia vidonge vyenye kichocheo kimoja?
Ikiwa jibu ni “Ndio”, kwa maswali yafuatayo, haupaswi kutumia vidonge vyenye kichocheo kimoja
- Je una sirosisi kali ya ini, ugonjwa wa ini, au uvimbe wa ini? (je macho au uvimbe wa ini? (je macho au ngozi yake ni ya manjano isivyo kawaida? [dalili za umanjano])
-
- NDIYO – Kama utaripoti kuwa na ugonjwa mkali wa ini (umanjano, hepatitisi amilifu, sirosisi kali, uvimbe wa ini), USITUMIE vidonge vyenye kichocheo kimoja. Daktari atakusaidia kuchagua njia isiyokuwa na vichocheo.
- Je kwa sasa una tatizo kubwa la damu kuganda kwenye miguu au mapafu yako?
-
- NDIYO- Kama utaripoti damu kuganda, USITUMIE vidonge vyenye projestini. Daktari atakusaidia uchague njia isiyokuwa na vichocheo.
- Je unatumia dawa kwa ajili ya kutibu kifafa? Je unatumia rifampicin kwa ajili ya kifua kikuu au ugonjwa mwingine?
-
- NDIYO -Kama unameza barbiturates, carbamazepine, oxcarbazepine, phenytoin, primidone, topiramate, au rifampicin, USITUMIE vidonge vyenye projestini. Vinaweza kupunguza nguvu za vidonge vyenye projestini. Daktari atakusaidia kuchagua njia nyingine lakini si vidonge vyenye vichocheo viwili au vipandikizi.
- Je una au umewahi kupata saratani ya matiti?
-
- NDIYO – USITUMIE vidonge vyenye projestini. Daktari atakusaidia uchague njia isiyokuwa na vichocheo.
Kwa kawaida wanawake wenye tatizo lolote kati ya hayo yaliyoorodheshwa hapa wasitumie vidonge vyenye kichocheo kimoja, hata hivyo, inapotokea kuwa hakuna njia nyingine sahihi zaidi au zinazokubalika, mtoa huduma mwenye utaalamu ambaye anaweza kuchunguza kwa makini hali ya mwanamke na mazingira anaweza kuamua kuwa anaweza kutumia vidonge vyenye kichocheo kimoja. Mtoa huduma anahitaji kuzingatia ugumu wa hali na kwa mazingira mengi, kama ataweza kuwa na nafasi ya kufuatilia
Wakati Gani wa Kuanza Kutumia Vidonge
Mwanamke anaweza kutumia vidonge vyenye kichocheo kimoja wakati wowote anapotaka kama kuna uhakika wa kutosha kuwa si mjamzito. Kama ataanza kutumia ndani ya siku 5 baada ya kuanza hedhi, hatahitaji njia mbadala ya kuzuia ujauzito. Kama ameanza kutumia baada ya siku 5 baada ya kuanza kupata damu ya hedhi atahitaji kutumia njia nyingine ya kuzuia ujauzito kwa angalau siku .
Hali ya mwanamke | Aanze lini kutumia |
Asiyepata hedhi | Unaweza kuanza kutumia vidonge vyenye kichocheo kimoja muda wowote kama kuna uhakika wa kutosha kuwa si mjamzito |
Unapaswa kuepa kushiriki ngono au kutumia njia nyingine ya uzazi wa mpango kwa angalau siku 2 zinazofuata | |
Aliyejifungua na Ananyonyenya | Unaweza kuanza kutumia vidonge vyenye kichocheo kimoja muda wowote (hata mara tu baada ya kujifungua) kama kuna uhakika wa kutosha kuwa si mjamzito |
Kama ni chini ya miezi 6 baada ya kujifungua, haujaanza kupata hedhi na unanyonyesha maziwa ya mama pekee – hauhitaji njia mbadala ya kukukinga na ujauzito | |
Kama umejifungua zaidi ya siku 21 zilizopita na haunyonyeshi wakati wote – mwanao anakula vyakula vingine – Unapaswa kuepa kushiriki ngono au kutumia njia nyingine ya uzazi wa mpango kwa angalau siku 2 zinazofuata | |
Aliyejifungua na hanyonyeshi | Unaweza kuanza kutumia vidonge vyenye kichocheo kimoja muda wowote (hata mara tu baada ya kujifungua) kama kuna uhakika wa kutosha kuwa si mjamzito |
Kama ataanza kutumia kabla ya siku 21 baada ya kujifungua – hatahitaji njia mbadala ya kuzuia ujauzito | |
Kama ataanza kutumia baada ya siku 21 baada ya kujifungua – Unapaswa kuepa kushiriki ngono au kutumia njia nyingine ya uzazi wa mpango kwa angalau siku 2 zinazofuata | |
Baada ya mimba kuharibika au kutoa mimba | Unatakiwa kuanza kutumia vidonge ndani ya siku 7 baada ya kuharibika kwa mimba |
Unapaswa kuepa kushiriki ngono au kutumia njia nyingine ya uzazi wa mpango kwa angalau siku 2 zinazofuata | |
Kubadili kutoka njia yenye vichocheo | Mara moja, kama amekuwa akitumia njia yenye vichocheo wakati wote na kwa usahihi au vinginevyo kukiwa na uhakika wa kutosha kuwa hana mimba. Hakuna haja ya kusubiri hedhi inayofuata. Hakuna haja ya kutumia kinga (kondomu). |
kubadili kutoka njia isiyo ya vichocheo | Anaweza kuanza kutumia vidonge vyenye kichocheo kimoja wakati wowote kukiwa na uhakika wa kutosha kuwa hana mimba. Atahitaji kinga kwa siku 2 za kwanza za kumeza vidonge |
Baada ya kumeza vidonge vya dharura kuzuia mimba | Anaweza kuanza kumeza vidonge vyenye projestini siku moja baada ya kumaliza kumeza vidonge vya dharura kuzuia mimba. Hakuna haja ya kusubiri hedhi inayofuata ili kumeza vidonge vyake. |
Mtumiaji mpya wa vidonge vyenye projestini aanze paketi mpya. | |
Mtumiaji anayeendelea ambaye anahitaji vidonge vya dharura kuzuia mimba kutokana na kukosea kumeza vidonge anaweza kuendelea pale alipoacha paketi aliyonayo. | |
Wanawake wote watahitaji kutumia kinga kwa siku 2 anapomeza vidonge. |
Namna ya kutumia vidonge
1. Utapewa vidonge | Unaweza kupatiwa paketi nyingi iwezekanavyo – hata za kutosha mwaka mzima (paketi 11 au 13). |
2. Angalia paketi ya vidonge ni ya aina gani? | Je, pakiti ni ya vidonge 28 au vidonge 35? |
Vidonge vyote kwenye paketi vina rangi inayofanana na vyote vinafanya kazi, kwa kuwa vina kichocheo ambacho huzuia mimba. | |
Utaoneshwa namna ya kumeza kidonge cha kwanza kutoka kwenye paketi na kisha jinsi ya kufuata maelekezo au mishale kwenye paketi ili kumeza vidonge vilivyobakia. | |
3. Maelezo muhimu | Meza kidonge kimoja kila siku — mpaka paketi iishe. |
Husisha umezaji wa vidonge na shughuli za kila siku – kama vile kupiga mswaki – inaweza kukusaidia kukumbuka. | |
Kumeza vidonge wakati unaofanana kila siku husaidia kuvikumbuka. Pia inaweza kusaidia kupunguza baadhi ya madhara | |
4. Jinsi ya kuanza paketi inayofuata | Utakapomaliza paketi moja, meza kidonge cha kwanza katika paketi inayofuata siku inayofuata. |
Ni muhimu sana kuanza paketi inayofuata kwa wakati. Kuchelewa kuanza paketi huleta hatari ya kupata mimba. | |
5. Fahamu jinsi ya kutumia njia mbadala | Wakati mwingine unaweza kuhitaji kutumia njia mbadala, kama vile wakati ukikosa kumeza vidonge. |
Njia mbadala ni pamoja na kuacha kufanya ngono, kondomu za kiume au kike, dawa za povu na jeli, na kumwaga nje. |
Jambo la kufanya kuhusu vidonge vilivyosahauliwa
Ni rahisi kusahau kumeza kidonge au kuchelewa kumeza vidonge vyenye projestini. Ni vizuri kujua nini cha kufanya unaposahau kumeza vdonge. Kama mwanamke akichelewa kumeza vidonge saa 3 au zaidi au akikosa kumeza kabisa, afuate maelekezo haya.
Ujumbe muhimu | Meza kidonge cha kichocheo ulichosahau mapema iwezekanavyo. |
Endelea kumeza vidonge kama kawaida, kimoja kila siku (Unaweza umeza vidonge 2 kwa wakati mmoja au katika siku moja) | |
Je unapata hedhi kama kawaida? | Kama ndiyo, pia utumie kinga kwa siku mbili zinazofuata. |
Pia, kama ulifanya ngono katika siku 5 zilizopita, unaweza kufikiri kumeza vidonge vya dharura kuzuia mimba | |
Kutapika au kuharisha kupita kiasi | Kama utatapika ndani ya saa 2 baada ya kumeza kidonge, meza kidonge kingine kutoka kwenye paketi haraka iwezekanavyo, kisha aendelee kumeza vidonge kama kawaida. |
Kama kutapika au kuharisha kutaendelea, fuata maelekezo ya jinsi ya kufanya kwa kutokana na kukosa kumeza vidonge hapo juu |
Imani potofu zilizopo kwenye jamii
Vidonge vyenye kichocheo kimoja:
- Havisababishi maziwa ya mama anayenyonyesha kukauka.
- Lazima vimezwe kila siku, iwe mwanamke amefanya au hajafanya ngono siku hiyo.
- Haziwafanyi wanawake kuwa wagumba.
- Haziwasababishi watoto wanaonyonya kuharisha.
- Hupunguza hatari ya mimba kutunga nje ya kizazi.
Leave feedback about this