Last Updated on October 13, 2023 by Dr Mniko
Vidonge Vyenye Vichocheo Viwili ni Nini?
Vidonge vyenye vichocheo viwili vina kiasi kidogo cha vichocheo vya aina mbili projestini na estrojeni vilivyo kama vichocheo vya asili vya projesteroni na estrojeni katika mwili wa binadamu. Vidonge hivi hufanya kazi hasa kwa kuzuia kuachiwa kwa mayai kutoka kwenye ovari (uovuleshaji).
Mambo Muhimu
Meza kidonge kimoja kila siku. Ili kupata mafanikio makubwa mwanamke lazima ameze vidonge kila siku na kuanza pakiti mpya ya dawa kwa wakati.
Kubadilika kwa hedhi ni kawaida lakini hakuna madhara. Kwa kawaida mwanamke hupata hedhi isiyotabirika kwa miezi michache ya kwanza na kisha hupungua na baadaye kupata hedhi ya kawaida.
Meza kidonge ulichokosa kumeza haraka iwezekanavyo. Kukosa kumeza vidonge kunaleta hatari ya kupata mimba na kunaweza kufanya athari za dawa kuwa mbaya.
Vinaweza kutolewa kwa wanawake wakati wowote ili waanze kuvitumia baadaye. Kama itashindikana kugundua ujauzito, mtoa huduma anaweza kumpatia vidonge mwanamke ili avimeze baadaye, wakati atakapoanza kupata hedhi.
Vidonge vyenye vchocheo viwili vinafanya Kazi kwa Ufanisi Kiasi Gani?
Ufanisi unategemea mtumiaji: Hatari ya kupata mimba ni kubwa wakati mwanamke anapoanza pakiti mpya ya vidonge akiwa amechelewa siku 3 au zaidi, au akiacha kumeza vidonge vitatu au zaidi karibu na mwanzo au mwisho wa pakiti ya vidonge.
- Kwa kawaida, zinatokea karibu mimba 8 kwa kila wanawake 100 wanaotumia vidonge vyenye vichocheo viwili kwa mwaka wa kwanza. Hii ina maana kuwa wanawake 92 kati ya kila 100 wanaotumia vidonge vyenye vichocheo viwili hawatapata mimba.
- Iwapo kutatokea makosa ya kuacha kumeza vidonge, kutakuwa na mimba 1 kwa wanawake 100 wanaotumia vidonge vyenye vichocheo viwili kwa mwaka wa kwanza (3 kwa wanawake 1,000).
Kuhusu Athari za Dawa
Madhara yanayofahamika zaidi
- Katika miezi michache ya mwanzo, baadhi ya watumiaji wameripoti kupata hedhi wakati ambao haukutegemewa, hedhi kidogo na siku chache zaidi, hedhi isiyotabirika na wengine hawakupata hedhi kabisa.
- Maumivu ya kichwa,maumivu ya matiti, kizunguzungu, kichefuchefu, mabadiliko ya mhemko na chunusi (zinaweza kupungua au kuongezeka, lakini kawaida hupungua)
- Kwa watu wachache sana, shinikizo la damu linaweza kupanda – iwapo ongezeko linatokana na vidonge vyenye vichocheo viwili, shinikizo hushuka haraka baada ya kuacha kutumia Vidonge vyenye vichocheo viwili
Ufafanuzi kuhusu madhara haya
- Madhara haya si dalili za ugonjwa.
- Madhara mengi kwa kawaida hupungua au kukoma ndani ya miezi michache ya kuanza kutumia vidonge vyenye vichocheo viwili. Ni ya kawaida lakini baadhi ya wanawake hayawapati.
Fanya yafuatayo ukipata madhara haya
- Endelea kutumia vidonge vyenye vichocheo viwili. Kuacha kutumia vidonge huleta hatari ya kupata mimba na kunaweza kusababisha baadhi ya madhara kuongezeka.
- Meza kidonge wakati unaofanana kila siku ili kusaidia kupunguza kupata hedhi isiyotarajiwa na pia kusaidia kukumbuka.
- Meza vidonge wakati wa chakula au wakati wa kulala ili kuepuka kichefuchefu. Unaweza kurudi kutafuta msaadakwa daktari kama madhara yatakuwa yanamsumbua
Faida na Hasara za kutumia vidonge venye vichocheo viwili
Faida za Kiafya
- Husaidia kukulinda dhidi ya:
- Hatari ya kupata mimba
- Saratani ya kizazi
- Saratani ya ovari
- Dalili za Ugonjwa wa Uvimbe wa pelvisi (PID)
- Zinaweza kusaidia kukinga dhidi ya:
- Uvimbe wa ovari
- Anemia kutokana na Ukosefu wa madini ya chuma
- Hupunguza:
- Maumivu makali wakati wa hedhi,
- Matatizo ya kutokwa damu za hedhi,
- Maumivu wakati wa uovuleshaji,
- Nywele nyingi usoni na mwilini,
- Dalili za ugonjwa wa polycystic ovarian syndrome (hedhi isiyotabirika, chunusi, nywele nyingi usoni na mwilini), Dalili za endometriosisi (maumivu ya nyonga, hedhi isiyotabirika)
Hasara Kiafya
- Mara chache:
- Damu kuganda ndani ya mishipa ya miguu au mapafu (deep vein thrombosis au pulmonary embolism)
- Mara chache mno:
Nani Anaweza kutumia Vidonge vyenye vichocheo viwili
Karibu wanawake wote wanaweza kutumia Vidonge vyenye vichocheo viwili kwa usalama na inavyopasa, ikiwa ni pamoja na wanawake ambao:
- Wana watoto au hawajawahi kuwa nao
- Hawajaolewa
- Wa umri wowote, pamoja na vijana na wanawake wenye umri zaidi ya miaka 40
- Ambao wametoa mimba au mimba imeharibika
- Wanaovuta sigara—kama wana umri chini ya miaka 35
- Wana anemia sasa au walikuwa nayo siku za nyuma
- Wana vena varikosi
- Wameambukizwa VVU, kama wameanza au hawajaanza kutumia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI
Nani hawezi kutumi vidonge vyenye vichocheo viwili?
Ikiwa jibu ni “Ndio”, kwa maswali yafuatayo, haupaswi kutumia vidonge vyenye vichocheo viwili
- Je unamnyonyesha maziwa ya mama mtoto mwenye umri chini ya miezi sita?
- Kama ananyonyesha maziwa ya mama tu: Utapewa vidonge vyenye vichocheo viwili ili uanze kuvimeza miezi sita baada ya kuzaa au wakati maziwa ya mama yatakapokuwa si chakula kikuu cha mtoto—lolote litakalotangulia
- Kama atanyonyesha kiasi: Unaweza kuanza kutumia Vidonge vyenye vichocheo viwili mapema wiki 6 baada ya mtoto kuzaliwa
- Je unavuta sigara?
- Kama una umri wa miaka 35 au zaidi na anavuta sigara, usitumie Vidonge vyenye vichocheo viwili. tunashauri aache kuvuta sigara na tunamsaidie kuchagua njia nyingine
- Je unaugua sirosisi ya ini, ugonjwa wa ini, au uvimbe wa ini? (Je macho au ngozi yake ni ya njano isiyo kawaida? [Dalili za umanjano]) Umewahi kuugua umanjano wakati ukitumia Vidonge vyenye vichocheo viwili?
- Kama una ugonjwa mkali wa ini (umanjano, hepatitisi kali, sirosisi ya wastani au kali, uvimbe wa ini) au hata kama aliwahi kuwa na umanjano wakati akitumia Vidonge vyenye vichocheo viwili, usitumie Vidonge vyenye vichocheo viwili. Tutakusaidia kuchagua njia isiyotumia kichocheo (Anaweza kutumia sindano za kila mwezi kama alishawahi kupata umanjano alipotumia tu Vidonge vyenye vichocheo viwili.)
- Je una tatizo la shinikizo la juu la damu?
- NDIO – Kama huwezi kupima shinikizo la damu na umeripoti historia ya shinikizo la juu la damu, au kama unapata matibabu ya shinikizo la juu la damu, USITUMIE Vidonge vyenye vichocheo viwili. Nenda kupimwe shinikizo la damu kama inawezekana au daktari atakusaidia kuchagua njia isiyotumia estrojeni.
- Pima shinikizo la damu kama inawezekana: Kama shinikizo lako la damu litakuwa chini ya 140/90 mm Hg, utapatiwa Vidonge vyenye vichocheo viwili. Kama shinikizo la damu la sistoli ni 140 mm Hg au zaidi au shinikizo la damu la diastoli likiwa 90 au zaidi, HAUTAPEWA Vidonge vyenye vichocheo viwili. Utasaidiwa kuchagua njia isiyokuwa na estrojeni.
- Je umewahi kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari kwa zaidi ya miaka 20 au kuharibika mishipa ya damu, macho, figo, au mfumo wa neva kulikosababishwa na ugonjwa wa kisukari?
- NDIYO-Usitumie Vidonge vyenye vichocheo viwili. Daktari atakusaidia kuchagua njia nyingine isiyokuwa na estrojeni lakini isiwe sindano za projestini
- Je una ugonjwa wa kibofu cha nyongo kwa sasa au unatumia dawa za ugonjwa wa kibofu cha nyongo?
- NDIYO – Usitumie Vidonge vyenye vichocheo viwili. Daktari atakusaidia kuchagua njia nyingine lakini si kipandikizi au pete ya uzazi wa mpango
- Umewahi kupata kiharusi, damu kuganda miguuni au kwenye mapafu, moyo kushindwa kufanya kazi, au matatizo mengine makubwa ya moyo?
- NDIYO-Kama ataripoti moyo kushindwa kufanya kazi, ugonjwa wa moyo kutokana na kuziba kwa ateri au kuwa nyembamba, au kiharusi, HAUTAPATIWA Vidonge vyenye vichocheo viwili. Daktari atakusaidia kuchagua njia isiyokuwa na estrojeni lakini isiwe sindano za projestini. Kama umeripoti kuganda kwa damu kwenye vena za miguu au mapafu , UTASAIDIWA kuchagua njia isiyokuwa na kichocheo
- Je unayo au umewahi kupata saratani ya matiti?
- NDIYO- Hautapewa Vidonge vyenye vichocheo viwili. UTASAIDIWA kuchagua njia isiyokuwa na kichocheo
- Je unatumia dawa kwa ajili ya kutibu kifafa? Je unatumia rifampicin kwa ajili ya tibii au ugonjwa mwingine?
- NDIYO– Iwapo unatumia barbiturates, carbamazepine, oxcarbazepine, phenytoin, primidone, topiramate, au rifampicin, usipatiwe Vidonge vyenye vichocheo viwili. Zinaweza kufanya Vidonge vyenye vichocheo viwili vishindwe kufanya kazi. UTASAIDIWA kuchagua njia nyingine lakini isiwe vidonge vya projestini au vipandikizi.
- Je unapanga kufanya upasuaji mkubwa ambao utakufanya usitembee kwa wiki moja au zaidi?
- NDIYO- Kama ndivyo, unaweza kuanza kutumia Vidonge vyenye vichocheo viwili wiki mbili baada ya upasuaji. Kabla hajaanza kutumia Vidonge vyenye vichocheo viwili, atumie kinga
- Je una magonjwa mengine kadhaa ambayo yanaweza kukuongezea hatari ya kupata ugonjwa wa moyo (ugonjwa wa ateri koronari) au kiharusi, kama vile uzee, uvutaji wa sigara, shinikizo la juu la damu, au kisukari?
- NDIYO – Usitumie Vidonge vyenye vichocheo viwili. Daktari atakusaidia kuchagua njia isiyokuwa na estrojeni lakini isiwe sindano za projestini.
- Je imewahi kutokea wakati fulani ukashindwa kuona wakati kichwa kikiwa kinauma sana (kipandauso)? Je huwa unapata maumivu makali ya kichwa ya kugonga, mara nyingi upande mmoja wa kichwa, ambayo yanaweza kuendelea kuanzia saa chache hadi siku kadhaa na yanayoweza kusababisha kichefuchefu au kutapika (kipandauso)? Maumivu ya kichwa Kwa namna hiyo mara nyingi huzidishwa Na mwanga, kelele, au kutembea.
- NDIYO- Kama ulishapata kipandauso katika umri wowote, USITUMIE Vidonge vyenye vichocheo viwili. Daktari atakusaidia kuchagua njia isiyokuwa na estrojeni.
Kwa kawaida, wanawake wenye hali zilizoorodheshwa hapo juu inafaa wasitumie vidonge vyenye vichocheo viwili. Hata hivyo, katika hali ya kipekee, iwapo hakuna njia nyingine sahihi au haziwezekani kwake kutumia njia hiyo, mtoa huduma mwenye utaalamu ambaye anaweza kuchunguza kwa makini matatizo maalum na hali ya mwanamke huyo anaweza kuamua kama anaweza kutumia Vidonge vyenye vichocheo viwili. Mtoa huduma anahitaji kufikiria ukubwa wa tatizo lake na, kwa matatizo yaliyo mengi, kama ataweza kupata nafasi ya kufuatilia.
Wakati Gani wa Kuanza Kutumia Vidonge vyenye vichocheo viwili
Mwanamke anaweza kuanza kutumia Vidonge vyenye vichocheo viwili wakati wowote anapotaka kama kuna uhakika kuwa si mjamzito. Pia, mwanamke anaweza kupatiwa Vidonge vyenye vichocheo viwili wakati wowote na kuelezwa lini aanze kuvitumia.
Hali ya mwanamke | Aanze lini kutumia |
Ukiwa katika siku za hedhi | -Kama ataanza ndani ya siku 5 baada ya kuanza hedhi, hakuna haja ya kinga -Kama ni zaidi ya siku 5 baada ya kuanza hedhi, anaweza kuanza kutumia wakati wowote kukiwa na uhakika wa kutosha kuwa si mjamzito. Atahitaji kutumia kinga kwa siku saba za kwanza za kumeza vidonge |
Kunyonyesha wakati wote | -Utapewa Vidonge vyenye vichocheo viwili na uanze kuvitumia miezi sita baada ya kujifungua au wakati maziwa ya mama yanapokuwa si chakula kikuu cha mtoto – lolote linalotangulia. |
Asiyenyonyesha | –Chini ya wiki 4 baada ya kujifungua – Unaweza kuanza Vidonge vyenye vichocheo viwili wakati wowote kati ya siku za 21-28 baada ya kujifungua. Anza vidonge wakati wowote katika siku hizi 7. Hakuna haja ya kinga –Zaidi ya wiki 4 baada ya kujifungua – Unaweza kuanza Vidonge vyenye vichocheo viwili wakati wowote itakapokuwa dhahiri kuwa si mjamzito. Utahitaji kutumia kinga kwa siku 7 za mwanzo za kumeza vidonge. |
Kukosa hedhi (kusikohusiana na kuzaliwa kwa mtoto au kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama) | -Unaweza kuanza kutumia Vidonge vyenye vichocheo viwili wakati wowote itakapodhihirika wazi kuwa huna mimba. Utahitaji kutumia kinga kwa siku 7 za kwanza za kumeza vidonge |
Baada ya mimba kuharibika au kutoa mimba | -Mara moja. Atahitaji njia mbadala kwa siku 7 za kwanza za kumeza vidonge. |
Baada ya kumeza vidonge vya dharura vya kuzuia mimba | -Anaweza kuanza kutumia Vidonge vyenye vichocheo viwili siku moja baada ya kumaliza kutumia vidonge vya dharura vya kuzuia mimba -Kama ni mtumiaji mpya- utapaswa kuanza pakiti mpya ya vidonge. Kama n mtumiaji anayeendelea na ulisahau kumeza vidonge vyako – endelea na pakiti yako pale ulipoishiaWanawake wote watahitaji kutumia kinga kwa siku 7 za mwanzo wanapomeza vidonge |
Jinsi ya kutumia vidonge vyenye vichocheo viwili
Utapewa vidonge | Unaweza kupatiwa paketi nyingi iwezekanavyo – hata za kutosha mwaka mzima (paketi 13). |
Angalia paketi ya vidonge ni ya aina gani? | Je, paketi ni ya 21 au vidonge 28. Kwa paketi ya vidonge 28, vidonge 7 vya mwisho vina rangi tofauti na havina kichocheo. Utaoneshwa jinsi ya kumeza kidonge cha kwanza kutoka kwenye paketi na kisha jinsi ya kufuata maelekezo au mishale kwenye paketi kumeza vidonge vilivyobaki. |
Maelezo muhimu | Meza kidonge kimoja kila siku — mpaka paketi iishe. Husisha umezaji wa vidonge na shughuli za kila siku – kama vile kupiga mswaki – inaweza kukusaidia kukumbuka. Kumeza vidonge wakati unaofanana kila siku husaidia kuvikumbuka. Pia inaweza kusaidia kupunguza baadhi ya madhara |
Jinsi ya kuanza paketi inayofuata | Paketi za vidonge 28: Utakapomaliza paketi moja, chukua kidonge cha kwanza katika paketi inayofuata siku inayofuata. Paketi za vidonge 21: Baada ya kumeza kidonge cha mwisho katika paketi moja, subiri siku 7 – si zaidi – na kisha meza kidonge cha kwanza katika paketi inayofuata. Ni muhimu sana kuanza paketi inayofuata kwa wakati. Kuchelewa kuanza paketi huleta hatari ya kupata mimba. |
Fahamu jinsi ya kutumia njia mbadala | Wakati mwingine unaweza kuhitaji kutumia njia mbadala, kama vile wakati ukikosa kumeza vidonge. Njia mbadala ni pamoja na kuacha kufanya ngono, kondomu za kiume au kike, dawa za povu na jeli, na kumwaga nje. |
Jambo la kufanya kuhusu vidonge vilivyosahauliwa
Ni rahisi kusahau kumeza kidonge au kuchelewa kumeza kidonge. Ni vizuri kujua nini cha kufanya unaposahau kumeza vdonge.
Ujumbe muhimu | Meza kidonge cha kichocheo ulichopitisha mapema iwezekanavyo. Endelea kumeza vidonge kama kawaida, kimoja kila siku (Unaweza umeza vidonge 2 kwa wakati mmoja au katika siku moja) |
Kukosa kumeza kidonge 1 au 2? Kuchelewa kuanza pakiti mpya siku 1 au 2? | Meza kidonge cha kichocheo mapema iwezekanavyo. Kuna hatari kidogo au hakuna hatari kabisa ya kupata mimba |
Kukosa kumeza vidonge 3 au zaidi Kuchelewa kuanza paketi mpya siku 3 au zaidi? | Meza kidonge cha kichocheo mapema iwezekanavyo. Tumia njia mbadala kwa siku 7 zinazofuata. Pia, kama ulishafanya ngono siku 5 zilizopita, unaweza kufikiria kutumia Vidonge vya Dharura Kuzuia Mimba |
Kukosa kumeza vidonge visivyokuwa na kichocheo? (vidonge 7 vya mwisho kwenye paketi ya vidonge 28) | Tupa vidonge visivyokuwa na kichocheo ulivyoacha kumeza Endelea kumeza Vidonge vyenye vichocheo viwili, kimoja kila siku. Anza paketi mpya kama kawaida |
Kutapika au kuharisha kupita kiasi | Kama utatapika ndani ya saa 2 baada ya kumeza kidonge, meza kidonge kingine kutoka kwenye paketi haraka iwezekanavyo, kisha aendelee kumeza vidonge kama kawaida. Kama utaendelea kutapika au kuharisha kwa zaidi ya siku 2, fuata maelekezo ya kukosa kumeza kidonge 1 au 2, hapo juu |
Kwa nini Baadhi ya Wanawake Husema Wanapenda Vidonge vyenye vichocheo viwili
- Vinadhibitiwa na wanawake
- Vinaweza kuacha kutumiwa wakati wowote bila msaada wa mtoa huduma
- Haviathiri tendo la ngono
Kuweka Sawa imani potofu zilizopo kwenye jamii
Vidonge uzazi wa mpango:
- Havijai kwenye mwili wa mwanamke. Mwanamke hahitaji “kupumzika” kumeza Vidonge vya Vya Uzazi wa Mpango.
- Lazima vimezwe kila siku, hata kama mwanamke amefanya tendo la ngono au hakufanya siku hiyo.
- Havimfanyi mwanamke kuwa mgumba.
- Havisababishi matatizo ya uzazi au kuzaa watoto wengi.
- Havibadili tabia ya mwanamke kijinsia.
- Havikusanyiki tumboni.
- Badala yake, vidonge huyeyuka kila siku.
- Haviharibu ujauzito uliopo
Leave feedback about this