VIPANDIKIZI

Vipandikizi ni Nini?

Vipandikizi ni vijiti vidogo vya plastiki au kapsuli, kila kimoja kina ukubwa wa njiti ya kibiriti, ambacho hutoa vichocheo vya projestini vilivyo kama vichocheo vya asili vya projesteroni kwenye mwili wa binadamu.

 • Mtoa huduma ya afya aliyepata mafunzo maalum hufanya upasuaji mdogo kuingiza vipandikizi chini ya ngozi kwenye mkono wa mwanamke.
 • Havina estrojeni, na hivyo vinaweza kutumika wakati wote wa kunyonyesha na vinaweza pia kutumiwa na mwanamke ambaye haruhusiwi kutumia estrojeni.
 • Kuna aina nyingi za vipandikizi: –
  • Jadelle: vijiti viwili, hufanya kazi kwa miaka 5
  • Implanon: kijiti kimoja, hufanya kazi kwa miaka 3 (utafi ti unaendelea ili kuona kama kinaweza kufanya kazi kwa miaka 4)
  • Norplant: kapsuli 6, zimepangwa kufanya kazi kwa miaka 5 (tafi ti kubwa zimegundua kuwa zinafanya kazi kwa miaka 7)
  • Sinoplant: vijiti viwili, hufanya kazi kwa miaka 5
 • Kimsingi hufanya kazi kwa:
  • kutengeneza ute mzito kwenye shingo ya kizazi (ute huu huzuia mbegu za kiume zisikutane na yai)
  • huvuruga mzunguko wa hedhi, pamoja na kuzuia mayai kupevuka na kutoka kwenye ovary

Mambo Muhimu

 • Vipandikizi ni vijiti au kapsuli za plastiki ambazo huingizwa chini ya ngozi ya mkono.
 • Huzuia mimba kwa muda mrefu. Ina ufanisi mkubwa wa miaka 3 hadi 7, kutegemea aina ya vipandikizi, na vikitolewa uwezo wa kushika mimba hurudi haraka.
 • Vinahitaji mtoa huduma za afya aliyepata mafunzo maalum ya kuviingiza na kuvitoa. Mwanamke hawezi kuanza kuweka au kuacha vipandikizi mwenyewe.
 • Mara vipandikizi vikishaingizwa mteja hahitaji kufanya lolote.
 • Mabadiliko ya hedhi ni ya kawaida lakini hayana madhara. Kawaida, hedhi huchukua muda mrefu na haitabiriki katika mwaka wa kwanza, na kisha damu ya hedhi hupungua, hutoka mara kwa mara au huweza kupata

Vina Ufanisi Kiasi Gani

Moja ya njia zenye ufanisi zaidi na za muda mrefu:

 • Inaweza kutokea chini ya mimba moja kwa wanawake 1000 wanaotumia vipandikizi kwa mwaka wa kwanza (wanawake 5 kwa 10,000). Hii ina maana kuwa wanawake 9,995 kati ya 10,000 wanaotumia vipandikizi hawatapata mimba.
 • Bado kuna hatari kidogo ya mimba baada ya mwaka wa kwanza wa kutumia vipandikizi na kuendelea kipindi ambapo mwanamke anatumia vipandikizi.
  • Kwa miaka 5 ya kutumia Jadelle: Karibu mimba 1 kwa wanawake 100
  • Kwa miaka 3 ya kutumia Implanon: Chini ya mimba 1 kwa wanawake 100 (1 kwa wanawake 1,000)
  • Kwa miaka 7 ya kutumia Norplant: Karibu mimba 2 kwa wanawake 100.
 • Vipandikizi vya Jadelle na Norplant huanza kupoteza uwezo mapema kwa wanawake wenye uzito mkubwa:
  • Kwa wanawake wenye uzito wa 80 kg au zaidi, Jadelle na Norplant hupungua uwezo baada ya kutumiwa kwa miaka 4.
  • Kwa wanawake wenye uzito wa 70-79 kg Norplant hupungua uwezo baada ya miaka 5 ya kutumiwa.
  • Watumiaji hawa wanatakiwa kubadili vipandikizi vyao mapema

Uwezo wa kushika mimba baada ya vipandikizi kutolewa: Bila kuchelewa

Kuhusu Athari za Vipandikizi

Madhara yanayofahamika zaidi Hedhi isiyotabirika inayoendelea kwa zaidi ya siku 8 kwa wakati kwa mwaka wa kwanza.
Hedhi ya kawaida, mara chache, au kukosa hedhi kabisa.
Maumivu ya kichwa, maumivu ya tumbo, maumivu ya matiti na huenda kukawa na madhara mengine.
Ufafanuzi kuhusu madhara haya Madhara si dalili za ugonjwa.
Madhara mengi kwa kawaida hupungua au kukoma ndani ya mwaka wa kwanza.
Yanajulikana, lakini baadhi ya wanawake hayawapati.
Mteja anaweza kurudi kuomba msaada kama madhara yanambughudhi.
Fanya yafuatayo ukipata madhara haya Hedhi isiyotabirika (kupata hedhi wakati usiotarajiwa hali inayokuudhi – iburprofen 800 mg au mefenamic acid 500 mg mara 3 kila siku kwa siku 5,

Faida na Hasara za kutumia vipandikizi

Faida za Kiafya

 • Husaidia kukinga dhidi ya:
  • Hatari ya kupata mimba
  • Dalili za ugonjwa wa uvimbe wa nyonga
 • Huweza kusaidia kukinga dhidi ya:
  • Anemia kutokana na upungufu wa madini ya chuma

Hasara  Kiafya

 • Hakuna

Athari Zisizo za kawaida

Zisizo za kawaida:

 • Maambukizi wakati wa kuingiza vipandikizi (maambukizi mengi hutokea ndani ya miezi miwili ya mwanzo baada ya kuingiza vipandikizi)
 • Ugumu wa kutoa (nadra kama vimeingizwa kwa usahihi na mtoa huduma mwenye na ujuzi wa kuondoa)

Mara chache

 • Kutoka kwa vipandikizi (kutoka kwa vipandikizi mara nyingi hutokea ndani ya miezi minne baada ya kuingizwa

Nani Anaweza Kutumia Vipandikizi

Karibu wanawake wote wanaweza kutumia vipandikizi kwa usalama na ufanisi, ikiwa ni pamoja na wanawake ambao:

 • Wanao au hawajawahi kupata watoto
 • Hawajaolewa
 • Wa umri wowote, ikijumuisha vijana na wanawake wenye umri zaidi ya miaka 40
 • Ambao ndiyo kwanza wametoa mimba, mimba imeharibika, au mimba imetunga nje ya kizazi
 • Wanavuta sigara, bila kujali umri wa mwanamke au idadi ya sigara anazovuta
 • Wananyonyesha (kuanzia wiki 6 baada ya kujifungua)
 • Wana anemia sasa au walikuwa nayo siku za nyuma
 • Wana mishipa ya damu iliyojikunjakunja
 • Wameambukizwa VVU, kama wanatumia au la dawa za kupunguza makali ya UKIMWI

Nani hawezi kutumia vipandikizi?

Ikiwa jibu ni “Ndio”, kwa maswali yafuatayo, haupaswi kutumia vipandikizi

 1. Je unaugua sirosisi kali ya ini, ugonjwa wa ini, au uvimbe wa ini? (Macho au ngozi yako ni ya manjano mno? [dalili za umanjano]) NDIYO -Kama ameripoti kuwa na ugonjwa mkali wa ini (umanjano, hepatitisi, sirosisi kali, uvimbe wa ini), usimweke vipandikizi. Msaidie kuchagua njia isiyo na vichocheo.
 2. Je kwa sasa una tatizo kubwa la damu kuganda kwenye miguu au mapafu yako? NDIYO -Kama ataripoti kwa sasa tatizo la damu kuganda (si kuganda kidogo), usimweke vipandikizi. Msaidie kuchagua njia isiyo na vichocheo.
 3. Je unapata hedhi isiyotabirika isivyo kawaida kwako? NDIYO – Kama anapata hedhi isiyotabirika ambayo inaonyesha dalili za mimba au hali ya ugonjwa, vipandikizi vinaweza kusababisha ugumu wa kufanya uchunguzi au ufuatiliaji wa tiba yoyote. Msaidie kuchagua njia ya kutumia wakati hali hiyo ikichunguzwa na kutibiwa (isiwe sindano zenye kichocheo kimoja, au kitanzi chenye madini ya shaba au vichocheo). Baada ya matibabu, fanya uchunguzi tena kuhusu uwezekano wa kutumia vipandikizi.
 4. Je unatumia dawa za kifafa? Je unameza rifampicin kwa ajili ya kifua kikuu au ugonjwa mwingine? NDIYO- Kama anatumia barbiturates, carbamazepine, oxcarbazepine, phenytoin, primidone, topiramate, au rifampicin, usimweke vipandikizi. Dawa hizi zinaweza kufanya vipandikizi vishindwe kufanya kazi vizuri. Msaidie kuchagua njia nyingine lakini isiwe Vidonge vyenye Vichocheo Viwili au vidonge vyenye kichocheo kimoja.
 5. Je una au umewahi kupata saratani ya matiti? NDIYO- Usimwekee vipandikizi. Msaidie kuchagua njia isiyo na vichocheo.

Kwa kawaida mwanamke mwenye tatizo lolote kati ya yale yaliyoorodheshwa asitumieVipandikizi. Hata hivyo, katika hali maalum, inapokuwa hakuna njia nyingine sahihi au inayofaa kwake, mtoa huduma za afya mwenye utaalamu ambaye kwa kawaida anaweza kutathmini hali na mazingira maalum ya mwanamke anaweza kuamua kumpatia vipandikizi. Mtoa huduma za afya anaweza kufikiria ukubwa wa tatizo lake na, kwa matatizo mengi, kama ataweza kupata huduma za ufuatiliaji.

Uwekaji wa Vipandikizi

Mwanamke anaweza kuwekewa kipandikizi wakati wowote anapotaka kama kuna uhakika wa kutosha kuwa hana mimba. Kama atawekewa kipandikizi ndani ya siku 7 baada ya hedhi kuanza, hauhitaji njia nyingine kujikinga na mimba. Kama amewekewa kipandikizi siku 7 baada ya hedhi kuanza, unapaswa kuacha kushiriki ngono au kutumia njia nyingine ya kuzuia mimba kwa siku 7 zinazofuata ili kuipa muda sindano kuanza kufanya kazi.

Hali ya mwanamke Aanze lini kutumia
Asiyepata hedhi Kipandikizi huwekwa wakati wowote kama kuna uhakika wa kutosha kuwa hana mimba. unapaswa kuacha kushiriki ngono au kutumia njia nyingine ya kuzuia mimba kwa siku 7 zinazofuata ili kukipa kipandikizi kuanza kufanya kazi.
Aliyejifungua na Ananyonyesha Kipandikizi huwekwa wakati wowote kama kuna uhakika wa kutosha kuwa hana mimba.
Kama ananyonyesha wakati wote na ni chini ya miezi 6 baada ya kujifungua hahitaji kinga ya mimba. Kama hayanyosheshi wakati wote anapaswa kutumia kinga kwa siku 7
Aliyejifungua na hanyonyeshi Kipandikizi huwekwa wakati wowote (hata mara tu baada ya kujifungua) kama kuna uhakika wa kutosha kuwa hauna mimba.
Kama ni chini ya siku 21 baaada ya kujifungua hahitaji kinga, kama ni zaidi ya siku 21 baada ya kujifungua unahitaji kutumia kinga kwa siku 7 za mwanzo
Baada ya mimba kuharibika au kutoa mimba Kipandikizi kinaweza kuwekwa ndani ya siku 7 baada ya mimba kuharibika (hata baada tu ya mimba kutoka).
Unapaswa kuacha kushiriki ngono au kutumia njia nyingine ya kuzuia mimba kwa siku 7 zinazofuata ili kukipa kipandikizi kuanza kufanya kazi.
Kubadili kutoka njia yenye vichocheo Kipandikizi huwekwa wakati wowote kama kuna uhakika wa kutosha kuwa hana mimba na amekuwa akitumia njia yenye vichocheo kwa uangalifu
kubadili kutoka njia isiyo ya vichocheo Kipandikizi huwekwa wakati wowote kama kuna uhakika wa kutosha kuwa hana mimba
Unapaswa kuacha kushiriki ngono au kutumia njia nyingine ya kuzuia mimba kwa siku 7 zinazofuata ili kukipa kipandikizi kuanza kufanya kazi.

Namna ya Kuweka Vipandikizi

Taratibu za Kuweka Jadelle na Norplant

Kuingiza vipandikizi huchukua dakika chache tu lakini wakati mwingine inaweza kuchukua muda mrefu zaidi, kutegemeana na ujuzi wa mtoa huduma. Matatizo yanayohusiana na hili hutokea kwa nadra na pia hutegemeana na ujuzi wa mtoa huduma. (Implanon huingizwa kwa kutumia kifaa maalum kinachofanana na sindano. Haihitaji upasuaji.)

 1. Mtoa huduma anatumia taratibu sahihi za kuzuia maambukizi.
 2. Mwanamke anachomwa sindano ya ganzi chini ya ngozi ya mkono wake ili kuzuia maumivu wakati wa kuingiza vipandikizi. Sindano hii inaweza kuleta maumivu. Mwanamke anakuwa macho wakati wote wa shughuli hii.
 3. Mtoa huduma anapasua sehemu kidogo kwenye ngozi upande wa ndani wa mkono.
 4. Mtoa huduma anaingiza vipandikizi chini ya ngozi. Mwanamke anaweza kuhisi msukumo au mvuto wa ghafla
 5. Baada ya vipandikizi vyote kuingizwa, mtoa huduma anafunga sehemu aliyopasua kwa kutumia bendeji. Hakuna haja ya kushona. Sehemu iliyopasuliwa imefunikwa na kitambaa na mkono unafungwa na kitambaa cha shashi.

Kuondoa Vipandikizi

Watoa huduma hawatakataa au kuchelewa wakati mwanamke anapoomba kuondolewa vipandikizi vyake, bila kujali sababu zake, kama ni za kibinafsi au kitabibu. Wafanyakazi wote lazima waelewe na kukubali kuwa mtu asishinikizwe au kulazimishwa kuendelea kutumia vipandikizi.

 1. Mtoa huduma atumie taratibu sahihi za kuzuia maambukizi.
 2. Mwanamke huchomwa sindano ya ganzi chini ya ngozi ya mkono wake ili kuzuia maumivu wakati wa kuondoa vipandikizi. Sindano hii inaweza kuleta maumivu. Anabaki macho wakati wote wa utoaji.
 3. Mtoa huduma ya afya anapasua sehemu ndogo kwenye ngozi upande wa ndani ya mkono, karibu na mahali vilipoingizwa vipandikizi.
 4. Mtoa huduma anatumia kifaa kutoa kila kipandikizi. Mwanamke anaweza kuhisi mvuto wa ghafl a, maumivu kidogo, au mwasho wakati wa kutoa na kwa siku kadhaa baadaye.
 5. Mtoa huduma anafunga sehemu aliyopasua kwa bendeji. Hakuna haja ya kushona. Bendeji ya elastiki inaweza kuwekwa juu ya bendeji ili kushikilia kwa siku 2 au 3 na kupunguza uvimbe.

Kama mwanamke anahitaji vipandikizi vipya, vitawekwa juu au chini ya eneo vilipokuwa vipandikizi vya awali au kwenye mkono mwingine

Imani potofu zilizo kwenye jamii

Vipandikizi:

 • Huacha kufanya kazi mara vinapotolewa. Vichocheo vyake havibaki kwenye mwili wa mwanamke.
 • Vinaweza kusitisha hedhi, lakini hii haina madhara. Ni sawa na kukosa hedhi wakati wa ujauzito. Damu haijijengi ndani ya mwili wa mwanamke.
 • Havisababishi wanawake kushindwa kushika mimba.
 • Havihamii sehemu nyingine ya mwili.
 • Kwa kiasi kikubwa hupunguza hatari ya mimba kutunga nje ya kizazi.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/birthcontrol.html

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Jiunge Nasi