WENDAWAZIMU

 • August 17, 2020
 • 0 Likes
 • 147 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Wendawazimu (psychosis) ni hali ya kupoteza mawasiliano na ukweli, mara nyingi mgonjwa huwa na imani potofu kuhusu mambo yanayofanyika au mtu anayeyafanya na huanza kuona vitu au kisikia sauti ambazo watu wengine hawavioni au kuvisikia.

Dalili za wendawazimu ni nini?

Dalili za wendawazimu zinaweza kujumuisha:   

 • Mawazo yaliyovurugika na kunena kwa maneno yasiyopangiliwa vyema,kwa hiyo hayaeleweki vyema.
 • Dhana potofu ambazo hazijajengwa kwenye ukweli (delusion), hasa hofu na mashaka yasio na sababu/msingi wowote unaoeleweka.    
 • Kusikia, kuona, au kuhisi vitu ambavyo havipo (hallucinations)    
 • Mawazo ambayo “hurukaruka” kati ya mada moja hadi mada nyingine isiyohusiana (mfumo wa mawazo uliovurugika)

Wendawazimu husababishwa na nini?

 • Vitu kadhaa na hali fulani za kitabibu zinaweza kusababisha wendawazimu, ikiwa ni pamoja na:
  • Pombe na madawa fulani ya kulevya, yanaweza kusababisha wendwazimu wakati wa kuyatumia  au unapoyakosa.
  • Uvimbe kwenye ubongo
  • Ugonjwa wa Dementia (huu ni ugonjwa wa akili ambao husababisha mgonjwa kupoteza kumbukumbu,hulka ya mgonjwa hubadilika na hupata shida kufikiria) au Alzheimer( huu ni ugonjwa wa akili ambao husababisha kupungua kwa  uwezo wa kufikiria,ugonjwa huwapata wazee au watu walio kwenye umri wa kati)
  • Magonjwa yanayoharibu ubongo, kama ugonjwa wa Parkinson na ugonjwa wa Huntington
  • VVU na maambukizo mengine yanayoathiri ubongo
  • Dawa nyingine zinazotolewa na daktari , kama vile steroids na stimulants         
  • Aina fulani za kifafa        
  • Kiharusi    
 • Wendawazimu pia hutokea kama dalili ya magonjwa kadhaa ya akili, hii ni pamoja na:        
  • Bipolar disorder (ugonjwa huu husababisha mtu kufurahi au kuhuzunika kupita kiasi ,hisia zake hubadilika-badilika bila sababu maalumu)        
  • Delusional disorder (matatizo ya kurukwa akili yanayosababisha mgonjwa kuwa na maono/imani za uwongo)
  • Depression with psychotic features(kufadhaika moyo/kuvunjwa moyo/kushuka moyo/sonona yenye dalili za wendawazimu)
  • Skizofrenia (schizophrenia)

Wakati gani utafute matibabu haraka?

Piga simu kwa mtoa huduma wa afya au mtaalamu wa afya ya akili ikiwa wewe au mwanafamilia anaonesha dalili za kurukwa akili. Ikiwa kuna wasiwasi wowote kuhusu usalama wake, mpeleka mara moja kwenye kituo cha afya kilicho karibu akaonwe na daktari.

Utambuzi    

 • Tathmini na vipimo vya kisaikolojia hutumiwa kutambua sababu ya wendawazimu.    
 • Upimaji wa maabara na uchunguzi wa ubongo unaweza usihitajike, lakini wakati mwingine unaweza kusaidia kugundua sababu ya wendawazimu. Vipimo vyaweza kujumuisha:
  • Vipimo vya damu kuangalia viwango vya elekroliti (electrolyte) na viwango vya homoni mwilini       
  • Vipimo vya damu kuchunguza Kaswende na maambukizi mengine yanayoweza kusababisha kurukwa akili
  • Vipimo kuangalia kiwango cha madawa yaliyo kwenye damu
 • MRI ya ubongo (kupiga picha ya ubongo )

Uchaguzi wa matibabu    

 • Matibabu hutegemea sababu ya wendawazimu. Huduma inayotolewa hospitalini mara nyingi huhitajika ili kuhakikisha usalama wa mgonjwa.
 • Antipsychotic drugs (dawa za kudhibiti wendawazimu), ambazo hupunguza kuona vitu au kusikia sauti ambazo wengine hawazisikii, husaidia pia kupunguza imani potofu na kuboresha tabia na uwezo wa kufikiri mgonjwa, hata kama sababu ya wendawazimu ni ya kimwili au ugonjwa wa akili, dawa hizi husaidia.

Matarajio?    

 • Matokeo ya jinsi mgonjwa atakavyoendelea hutegemea sababu ya wendawazimu wake. Ikiwa sababu inaweza kusahihishwa, matarajio mara nyingi huwa mazuri, na matibabu kwa dawa za kudhibiti wendawazimu huwa kwa muda mfupi tu.
 • Hali zingine sugu, kama vile skizofrenia (schizophrenia), zinahitaji matibabu ya muda mrefu na dawa za kudhibiti wendawazimu (antipsychotics) ili kudhibiti dalili.

Matatizo yatokanayo na wendawazimu

Wendawazimu husababisha mtu kushidwa kufanya kazi za kawaida na hata hushindwa kujitunza mwenyewe. Ikiwa hali hii itasalia bila kutibiwa,mgonjwa anaweza kujidhuru mwenyewe au kuwadhuru wengine.

Kuzuia wendawazimu

Kuzuia wendawazimu hutegemea sababu yake. Kwa mfano, kuepuka kunywa pombe,kama wendwazimu umesababishwa na pombe kupita kiasi.

Chanzo

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/article/001553.htm

Leave Your Comment