YABISI KAVU

YABISI KAVU

 • January 13, 2021
 • 0 Likes
 • 18 Views
 • 0 Comments

Maelezo ya jumla

Ugonjwa wa yabisi-rkavu (arthritis) na hali nyingine 100 za yabisi-baridi (rheumatic) huathiri viungo na tishu zinazozunguka viungo. Makali ya ugonjwa na eneo la dalili hutofautiana kulingana na aina yabisi inayousababisha . Kwa kawaida, hali ya yabisi-baridi husababisha maumivu na kukakamaa kwa viungo. Dalili zinaweza kujitoza polepole au ghafla. Hali fulani za yabisi-baridi zinaweza pia kuathiri mfumo wa kinga ya mwili na viungo mbalimbali vya ndani vya mwili.
Aina ya yabisi-kavu inayopatikana kwa wingi inchini marekani na duaniani kote ni yabisi inayotokana na kusagika viungio (osteoarthritis)  ikifuatiwa na jongo (gout), na ugonjwa wa yabisi-baridi (rheumatoid arthritis). Hivi sasa, wastani wa Wamarekani milioni 46 waliripoti kuwa daktari wao aliwaambia wana ugonjwa wa yabisi-kavu, na idadi hii inatarajiwa kuongezeka.

Je, nini dalili za Yabisi kavu?

Sehemu na eneo la dalili zinaweza kutofautiana kulingana na aina ya yabisi kavu (arthritis). Kwa kawaida, watu wenye ugonjwa wa yabisi-kavu wanahisi maumivu na kukakamaa kwa viungo. Dalili za yabisi-kavu (arthritis) zinaweza kuanza polepole au ghafla. Yabisi-kavu mara nyingi ni ugonjwa sugu, dalili zinaweza kuja na kwenda, au kuendelea kuwepo kwa kitambo.

Je Ni nini husababisha yabisi kavu?

Yabisi-kavu husababishwa na kuharibika kwa gegedu (cartilage). Gegedu kwa kawaida hulinda viungo na kivifanya viwe laini ili vifanye kazi vyema. Gegedu pia husaidia kupunguza shinikizo kwenye viungo ,kwa mfano,mtu anapotembea shinikizo kubwa huwa kwenye viungo vya miguu,gegedu huisaidia mifupa kuhimili shinikizo hili. Bila kiwango cha kawaida cha gegedu au kama gegedu limeharibika, mifupa husagana na kusababisha maumivu makali,kuvimba na kukakamaa kwa viungo.
Kuvimba kwa viungo kunaweza kusababishwa na:

 • Magonjwa yanayosababishwa na mfumo wa kinga (autoimmune)- haya ni magonjwa yanayosababishwa na mfumo wa kinga kushambulia tishu za mwili kimakosa na kuziharibu    
 • Kuvunjika mifupa   
 • Kuchakaa kwa kawaida kwa viungo (baada ya kutumika muda mrefu)   
 • Maambukizi, kwa kawaida ni bakteria au virusi

Kwa kawaida, uvimbe wa viungo huondoka baada ya sababu iliyousababisha kuondoka au kutibiwa.Wakati mwingine uvimbe hauondoki. Hili linapotokea,una yabisi-kavu sugu (chronic arthritis). Yabisi-kavu inaweza kutokea kwa wanaume au wanawake. Yabisi inayotokana na kusagika viungio (Osteoarthritis) ndio aina ya yabisi- kavu inayowapata watu wengi zaidi.

Kuna aina nyingi za yabisi-kavu,kila aina ina sababu yake,zifuatazo ni aina mbalimbali za yabisi-kavu:

 • Ankylosing spondylitis –Ni aina ya yabisi inayoathiri uti wa mgongo,hasa vijana ,husababisha kukakamaa kwa mgongo baadae
 • Gonococcal arthritis – yabisi-kavu inayosababishwa na gono
 • Gout (jongo)
 • Juvenile rheumatoid arthritis –Hii ni aina ya yabisi-baridi inayowapata watoto,uharibifu wa viungo husababishwa na kinga ya mwili
 • Other bacterial infections (nongonococcal bacterial arthritis)
 • Psoriatic arthritis
 • Reactive arthritis (Reiter syndrome)
 • Rheumatoid arthritis(in adults)
 • Scleroderma
 • Systemic lupus erythematosus (SLE)

Nani yuko kwenye hatari zaidi?

Sababu fulani zinahusishwa na hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa yabisi-kavu. Baadhi ya mambo haya yanaweza kurekebishwa na mengine hayawezi kurekebishwa.

Sababu zisizoweza kubadilika:

 • Umri: Hatari ya kupata yabisi-kavu huongezeka kadri umri unavyoongezeka.    
 • Jinsia: Aina nyingi za yabisi-kavu huwapata zaidi wanawake kuliko wanaume, 60% ya watu wenye yabisi-kavu ni wanawake. Jongo (gout) inawapata zaidi wanaume kuliko wanawake.    
 • Jenetiki: Jeni (gene) maalum huhusishwa na hatari kubwa ya aina fulani za ugonjwa wa yabisi-kavu, kama vile rheumatoid arthritis ,systemic lupus erythematosus ,na ankylosing spondylitis.

Sababu zinazoweza kubadilika

 • Kupunguza uzito na kitambi: uzito mkubwa unaweza kuchangia kutokea kwa yabisi-kavu kwenye magoti.    
 • Majeraha/Kuumia kwenye viungo: Uharibifu kwenye kiungo unaweza kuchangia kutokea kwa yabisi-kavu kwenye kiungo hicho.   
 • Maambukizo: Maambukizi ya vimelea yanaweza kuharibu gegedu na hatimaye kusababisha yabisi-kavu .  
 • Kazi: Kazi fulani zinahitaji mtu kupiga magoti na kuchuchumaa mara nyingi na kwa kurudiarudia,kazi za aina hii husababisha kudhoofika kwa maungio na tishu kulika, hili hupelekea kutokea kwa yabisi-kavu kwenye magoti.

Wakati gani utafute matibabu ya haraka?

Ikiwa una maumivu, kukakamaa, au uvimbe ndani au karibu na kiungo kimoja au zaidi,  mwone daktari. Ni muhimu kukumbuka kwamba kuna aina nyingi za ugonjwa wa yabisi-kavu,na utambuzi wa aina maalum uliyonayo utasaidia kumwongoza daktari ili upate matibabu sahihi. Kwa aina nyingi za yabisi-kavu hakuna tiba inayoweza kuponya kabisa,lakini uchunguzi wa mapema na matibabu sahihi ni muhimu. Utambuzi wa mapema na matibabu sahihi unaweza kupunguza maumivu na uharibifu zaidi wa viungo. Kadri unavyotambua mapema kuhusu yabisi-kavu ndipo utakapoanza matibabu mapema na kufanya mabadiliko kwenye mfumo wa maisha ili kusaidia kutibu yabisi yako.

Utambuzi

Mtoa huduma ya afya atafanya uchunguzi wa mwili na kuuliza maswali kuhusu historia ya matibabu yako.

Uchunguzi wa mwili unaweza kuonesha:

 • Majimaji kuzunguka kiungo
 • Viungo vinaweza kuwa na joto, vyekundu,na vinauma vikishikwa/kubonyeza
 • Viungo vitakua vimekakamaa,vigumu kujongea ,na wakati mwingine kusababisha maumivu.

Aina fulani za yabisi-kavu zinaweza kusababisha ulemavu wa viungo. Hii inaweza kuwa ishara ya ugonjwa mkali wa yabisi-baridi (rheumatoid arthritis ) ambao haukutibiwa vyema.
Vipimo vya damu na x-rays za viungo mara nyingi hufanyika ili kuchunguza kama kuna maambukizi au sababu nyingine zinazosababisha yabisi-kavu.
Daktari anaweza pia kuchukua sampuli ya maji yaliyo kwenye viungo kwa kuchoma shindano na kuyapeleka maabara kwa ajili ya vipimo

Uchaguzi wa matibabu

Lengo la matibabu ya yabisi-kavu ni kudhibiti maumivu, kupunguza uharibifu viungo, na kuboresha au kudumisha kazi ya viungo na ubora wa maisha. Kulingana na American College of Rheumatology, matibabu ya ugonjwa wa yabisi-kavu huhusisha yafuatayo:

 • Madawa
 • Tiba ya mazoezi ya viungo au Tiba ya kazi
 • Kitata (splint) na vifaa vya kusaidia kiungo kuhimili uzito
 • Elimu kwa mgonjwa na usaidizi
 • Kupunguza uzito
 • Upasuaji

Nini cha kutarajia

Matatizo machache yanayohusiana na ugonjwa wa yabisi-kavu yanaweza kutibiwa na kuponywa kabisa kwa matibabu sahihi.

Hata hivyo aina nyingi za ugonjwa wa yabisi kavu ni sugu,ni hali za muda mrefu.

Matatizo yanayoweza kutokea

matatizo ya ugonjwa wa yabisi-kavu ni pamoja na:

 • Maumivu ya muda mrefu
 • Ulemavu
 • Kushindwa/Ugumu wa kufanya kazi za kila siku ,,, kipara

Jinsi ya kuzuia yabisi kavu

Kwa kuzingatia aina ya yabisi-kavu, kuna hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa ili kupunguza hatari ya kuupata ugonjwa wa arthritis (yabisi-kavu).

 • Kudumisha uzito wa mwili ulio sahihi hupunguza maradufu hatari ya kupata yabisi inayotokana na kusagika viungio (osteoarthritis) na jongo (gout).
 • Kulinda viungo vyako visipate majeraha
 • Usitumie vibaya viungo vyako,tafuta namna ya kuifanya kazi yako bila kuchosha sana viungo.

Vyanzo

 • Share:

Leave Your Comment